Breaking News

Wanawake, Vijana Wahamasishwa Kushiriki Uongozi.



Na Abdul Sakaza
Wanawakevijana, wakiwemo wenye ulemavu, wametakiwa kutumia fursa za mafunzo ya uongozi kujijengea uwezo, kujiamini na kuongeza ushiriki wao katika nafasi za uongozi na maamuzi, sambamba na kuondoa vikwazo vinavyowafanya wanawake kutoshiriki kikamilifu katika uongozi.

Wito huo umetolewa mtaalamu wa ufuatiliaji na tathmini TAMWA-ZNZ Muhammed Khatib Muhammed kwa niaba ya Mkurugenzi wa Chama hicho Nairat Abdulla Ali wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne ya uongozi kwa vijana wanawake, yenye lengo la kuwawezesha kushiriki katika uongozi, uwajibikaji na demokrasia, kupitia mradi wa (We Lead) unaotekelezwa kwa ushirikiano na UN Women.

Muhammed ameelezakuwa Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za kuwaandaa wanawake vijana kushika nafasi za uongozi katika taasisi mbalimbali, vyama vya siasa na maeneo mengine ya kutoa maamuzi, kwa kuwajengea ujuzi, ujasiri na uwezo wa kuwasilisha mawazo yao pamoja na kushiriki katika mijadala inayohusu maendeleo ya jamii. 



Aidha amesema kuwa baada ya mafunzo, washiriki wanatarajiwa kupata fursa za kufanya mazoezi ya vitendo katika maeneo mbalimbali kwa kipindi cha miezi mitatu, hatua wasaidia kutumia maarifa waliyoyapata katika mazingira halisi ya uongozi na utendaji.
Mkufunzi wa mafunzo hayo Salmin Amour Mohammed amesema ni wakati wa vijana wa kike hususan wenye ulemavu kuiaminisha jamii kwa vitendo kuwa viongozi sio lazima wawe wanaume bali hata wanawake wanaweza kufanya vizuri zaidi ya hata wanaume. Huku akieleza kuwa kufanya hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa mila potofu kuhusu uongozi wa kijana mwanamke.


Aidha amewataka  wanawake na vijana wa kike kufuatilia ndoto zao bila kukata tamaa, akisisitiza kuwa ushiriki wao katika uongozi ni muhimu katika kuleta maendeleo na kutumia ipasavyo uwezo walionao katika jamii.



Katibu wa Wilaya ya Mjini, UVCCM Zanzibar, Lulu Alai Abdallah, ambae ameshiriki katika mafunzo hayo amewahimiza wanawake na vijana wa kike kujitokeza kushiriki katika nafasi za uongozi na kutumia uwezo wao kuchangia maendeleo ya jamii.
Ameeleza kuwa  mafunzo hayo yamemsaidia kuelewa misingi ya uongozi bora, kuboresha mawasiliano na viongozi, mashirika mbalimbali pamoja na wananchi, pamoja na  kumjengea uwezo wa kujiamini na kuzungumza mbele ya watu.


Lulu alisema wanawake wana uwezo wa kufanya kazi mbalimbali za maendeleo kama wanaume, ikiwemo uhandisi, udaktari na uongozi, hivyo wanapaswa kuondokana na dhana inayowafanya wajione kuwa kazi zao ni za nyumbani pekee

Sabrina Faki hamad kutoka Jumuiya ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA) amesema mafunzo hayo yamemjenga kujiamini kugombea nafasi yoyote ya uongozi bila kujali yake ya kijinsia na ulemavu, Aidha amewaasa vijana wa kike kuwa mstari wa mbele kujitokeza kugombania nafasi za uongozi.

Rhma abeid Awadh kutoka Jumuiya ya elimu vijana kaskazini Unguja amesema mafunzo hayo yamemjengea uwezo wa kutetea haki za wengine, sambamba na kupata mbinu za kuwa kiongozi , ikiwemo kuongoza bila kujali jinsi au jinsia ya mtu. (Usawa wa kijinsia), kuwa na maadili, na kuleta mabadiliko katika jamii.
kwa upande wake Bahati Ramadhan Hassan mwanafunzi kutoka chio Cha Tatifa Cha Zanzibar (SUZA) amesema mafunzo hayo yamemjengea uelewa kuwa kuzaliwa mwanamke sio udhaifu katika kutoa maamuzi, bali ana uwezo wa kufanya mengi mazuri katika uongozi. aidha ameeleza kuwa ili kutekeleza uongozi kivitendo ataanza kuwa mfano katika familia, skuli kwa wanafunzi pamoja na walimu wenzake.
Mradi huo ulioanza Machi 2026 na unatarajiwa kukamilika Desemba 2027, unalenga kuwapatia vijana 50 mafunzo katika awamu ya kwanza, wakiwemo wasichana 30 na wavulana 20, kwa lengo la kuwajengea uelewa wa pamoja kuhusu umuhimu wa uongozi jumuishi na usawa katika kushiriki kwenye nafasi za maamuzi.
Aidha, mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano na taasisi za elimu ya juu zikiwemo Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), katika kuandaa miongozo na kozi fupi za uongozi zitakazosaidia kuimarisha ujuzi na uwezo wa vijana katika masuala ya uongozi.

2 comments: