Breaking News

''ACHENI PLASTIKI, TUMIENI VYOMBO VYA ASILI KWA AFYA NA UCHUMI ENDELEVU'' WAJASIRIAMALI KIKUNDI CHA KAMBA NDEFU.

 


Na Said Khamis

Wananchi wametakiwa kuacha kutumia vyombo vya plastiki na vyombo vya bati na badala yake wawe na  utamaduni wa kutumia vyombo vya asili hususani kwa matumizi ya kupikia ikiwemo vyungu na mikungu.

‎Ushauri huo umetolewa na mjasiriamali wa kazi za mikono (Ufinyanzi) kutoka kikundi cha kamba ndefu group Bi Mariam Mohammed wakati Akizungumza na IKHUAN MEDIA huko Fuoni Wilaya ya Magharib B,alisema utumiaji wa vyombo vya bati kama vile sufuria husababisha kuchuja kemikali ambazo huleta madhara katika mwili wa binadamu.

‎Bi Mariam ameeleza kuwa watu wengi hivi sasa hawana utamaduni wakupikia kwenye vyungu kama ilivyokua zamani hivyo kuwepo kwa hali hiyo nimoja ya sababu inayopelekea watu wengi kupata maradhi ya matumbo.

‎"Zamani bibi zetu na mama zetu walikua hawatumii masufiria wakati wakupikia nawala walikua hawatumii ndoo za plastiki kwa ajili ya kutilia maji walikua wanatumia mitungi ambayo ilifinyanziwa na udogo " alisema Bi Mariam



‎Aidha Mjasiriamali huyo amewaomba wanawake kuachakua tegemezi kwa familia zao na badala yake wajishughulishe na shughuli za ujasiriamali ikiwemo ufinyanzi na kazi nyengine ili wajikwamue kiuchumi.

‎Alisema wanawake wanatikiwa kujitoa kujifunza kazi za mikono huku akiwataka kutumia maonesho mbali mbali yanayoandaliwa kuzitangaza bidhaa zao.

‎Sambamba na hayo baadhi ya wajasiliamali wanaofanya kazi katika kikundi hicho wameiomba jamii kujihusisha na ujasiriamali wa kazi za mikono ili kupanua soko la utalii nchini.

‎"Tutapo jikusanya pamoja na kutengeza bidhaa zetu tunaweza kupanua soko la utalii nchini na kuweza kujiongezea kipato " walisema Wanakikundi hao



‎Kikundi cha kamba ndefu group kinajishughulisha na utengenezaji wa bidhaa mbali mbali za kazi za mikono ikiwemo Vyungu, mikungu,mikoba ya ukili,vikapu, pawa, mbuzi za kukunia nazi,mikeka pamoja na bidhaa nyengne za asili.


No comments