TANZANIA KUSAFIRISHA MAHUJAJI ZAIDI YA 4,000 MWAKA 2026.
Na Said Khamis-10/12/2025
Waumini wa dini ya kiislam wenye nia ya kwenda kutekeleza ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia mwaka 2026 miladiya sawa na mwaka 1447 Hijiria wametakiwa kujisajili mapema na kufanya malipo ilikuweza kutekeleza ibada hiyo kwa ufanisi.
Rais wa Ofisiya Hijja Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Alhajj Abdulla Twalib Abdulla ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya Ibada ya Hijja Nchini Saudi Arabia kwamwaka 2026 sawa 1447 Hijiria huko katika ukumbi wa Msikiti wa Jamii Zinjibar Mazizini.
Amesema Ofisiya Hijja ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inatarajia kusafirisha jumla ya mahujaji watarajiwa Elfu Nne kwenda kutekeleza Ibada ya Hijja kwa mwaka 2026 miladiya sawa mwaka 1447 Hijiria kutoka Tanzania ambapo Zanzibar watasafirisha mahujaji Elfu Mbili na Mia Sita na kwaupande wa Tanzania Bara watasafirisha jumla ya mahujaji Elfu Mmoja na Mia Nne.
‘’Mahujaji hao elfu nne wataambatana na viongozi 40 katika yao 26 watakua wanahusiana na masuala ya utawala na uwendeshaji, viongozi kumi watu wa afya, na viongozi 4 watakua watu wahabari’’ alisema Alhajj Abdulla
Pia Alhajj Abdalla amesema katika mwezi wa Novemba tayari Ofisi hiyo imekamilisha maandalizi ya msingi ikiwemo kutiliana saini mkataba na Wizara ya Hijja na Umra ya Nchini Saudi Arabia hivyo mahujaji hao wanahimizwa kukamilisha matayarisho mapema na kuanza matayarisho ya hijja 2027/1448.
Aidha Alhajj Abdalla ameeleza kuwa Tanzania imepewa nafasi ya kupeleka zaidi ya Mahujaji Elfu Ishirini na Tanona Mia Tano lakini bado idadi hiyo haijatumi kakikamilifu hivyo ni vyema kwa waislam wenyeu wezo kutekeleza ibada hiyo kwani ibada ya hijja imefaradhishwa kwa wale wenye uwezo.
.jpeg)


No comments