Wananchi wametakiwa kufanya shughuli za ufugaji wa nyuki ili kupata kipato
Na Said Khamis.
Wananchi wametakiwa kufanya shughuli za ufugaji wa nyuki ili kupata kipato cha kuweza kujimu na familia zao.
Ushauri huo umetolewa na Katibu wa kikundi cha Ufugaji wa Nyuki cha Wema Kazi kilichopo Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Bw. Simai Jabu Vuai wakati akizungumza na Ikhuan Media. Amesema ufugaji wa nyuki unafaida nyingi ikiwemo kujipatia fedha pamoja na kutunza mazingira ili yaweze kubaki salama.
Amesema Nyuki si adui wa mwanadam kama baadhi ya watu wanavyodhani Bali ni rasilimali muhimu katika jamii inayohitaji kutunzwa na kuenziwa hususani kwa kuyafanya mazingira yaliyotuzunguka kuweza kubaki salama.
"Baadhi ya watu huamini kuwa nyuki ni adui wa mwanadamu wakati anapomuua lakini sivyo Nyuki wanatakiwa kutunzwa ili wasitoweke katika jamii kwa maslahi yetu na vizazi vyetu maana kuna faida nyingi tunazipata ikiwemo asali,fedha na hata kuyatunza mazingira. Alisema Katibu
Pia Bw.Simai ameeleza kuwa mizinga waliyo kopeshwa na serikali bado inachangamoto kubwa kwani nyuki wanaoingia ni kidogo pia haidumu kitokana na namna ilivyotengenezwa.
"Utakuta kwenye mzinga nyuki wanaingia lakini kidogo sana na isitoshe hawadumu hivyo hushindwa kuzaliana na kuzalisha asali kwa wingi hatujui tatizo ni nini kama mizinga au maeneo tunayofugia si rafiki " alisema Bw Simai
Akizungumzia changamoto ya uharibifu na wizi wa mizinga amesema baadhi ya wafugaji huzikata kamba wanazofungia mizinga na kufungia wanyama wao na wengine huiba mizinga hiyo jambo linalowarejesha nyuma kimaendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama wenzake mjumbe wa kikundi hicho Warda Suleiman Ali alisema licha ya kuwepo uharibifu wa mizinga na wizi lakini bado wadudu waharabifu wanawashambulia nyuki hao na kupelekea Nyuki kukimbia.
"Wadudu waharibifu wanaishambulia mizinga yetu na kupelekea Nyuki kukimbia lakini tayari malalamiko hayo tumeshayapeleka sehem husika lakini bdo hayajapatiwa ufumbuzi " alisema Mjumbe
Sambamba na hayo amesema licha ya kupata faidha mbalimbali katika ufugaji huo lakini bado wanakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi ikiwemo mizinga ya kufugia, glavu na hata mavazi ya kuvunia asali.
Lita moja ya asali huuzwa shilingi elfu 20 na mzinga mmoja wa nyuki huzalisha asali zaidi ya lita kumi.
No comments