USHIRIKIANO MDOGO KATI YA WAZAZI NA UONGOZI WA SHEHIA WACHOCHEA WATOTOKUJIINGIZA KATIKA UVUVI UNGUJA UKUU”
Na Said Khamis.
Kuwepo kwa mashirikiano madogo baina ya Wazazi na Afisi ya shehia Unguja Ukuu nimoja ya sababu inayopelekea baadhi ya watoto kujiingiza katika shughuli za uvuvi wakiwa katika umri mdogo.
Akizungumza na Ikhuan Media Mjumbe wa Sheha wa Shehia hiyo Seif Masoud Hassan alisema, baadhi ya Wazazi huwaachia watoto wao kujiingiza katika shughuli za uvuvi jambo ambalo hupelekea watoto hao kukosa haki zao za msingi ikiwemo Elimu.
Seif alieleza kwamba watoto wengi wenye umri mdogo hujiingiza katika shughuli za uvuvi ikiwemo kuvua, kupara samaki na hata kupiga pweza ili kuweza kupata kipato cha kujikumu na familia zao.
"Tunafahamu kuwa maisha ya wanakijiji wa Unguja ukuu ni magumu lakini wazazi tunatikiwa kuchukua jitihada za makusudi ili watoto wetu waweze kusoma skuli na madrasa " alisema Mjumbe huyo
Pia ameongeza kusema kuwa baadhi ya Wazazi huwaachia watoto wao kwamakusudi ili kuweza kusaidiana kuendesha familia zao jambo ambalo linamkosesha mtoto kupata haki yake ya elimu.
Kwa upande wa wazazi Wa watoto hao wamesema wamechukua jitihada mbalimbali kuhakikisha watoto wanakwenda skuli na madrasa lakini kutokana na hali duni walizonazo kwa baadhi kwabaadhi ya familia hulazimika watoto kufanya kazi hiyo.
"Hali zetu ni duni sana hatuna uwezo wa kuhudumia kila kitu familia zetu hivyo tunaona mtoto anapokua Mkubwa na yeye tunaanza kumrithisha kazi za uvuvi ili aweze kujitegemea" walisema wazazi
Sambamba na hayo wazazi hao wamewaomba wazazi wenzao kuwahimiza watoto wao kusoma ili kutimiza ndoto zao licha ya kuwa na halingumu za kimaisha kwani watoto ni taifa la kesho.



No comments