WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR WAPIGWA MSASA KUANDIKA HABARI ZA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WASICHANA.
Na Fatma Rajab.
Waandishi wa habari wametakiwa kutumia kalamu zao kwa kutoa uwelewa kuhusiana na athari za udhalilishaji dhidi ya wanawake na wasichana katika jamii.
Akizungumza katika mafunzao ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu kuripoti vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na wasichana kupitia mradi wa Tunaweza pamoja kumaliza udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana huko Tunguu wilaya ya kati unguja Afisa program kutoka TAMWA-ZNZ Asia Hakim Makame, amesema waandishi wa habari ni watu muhimu katika jamii hivyo ni vyema kutoa elimu kwa jamii ili waweze kufahamu athari za vitendo vya udhalilishaji na waweze kuripoti sehemu husika endapo watakutana navyo ili kuweza kupatiwa hukumu stahiki kwa atakaebainika kuhusika na udhalilishaji huo.
Aidha amesema mradi huo utatekelezwa katika maeneo ambayo udhalilishaji hutokea kwa kiasi kikubwa ikiwemo masokoni, maeneo ya usafirishsji, sehemu za uvuvi na biashara za mama ntilie ambapo wanawake na wasichana hudhalilishwa kwa kiasi kikubwa hivyo elimu hiyo itasaidia kupunguza udhalilishsji huo kutokea.
Kwa upande wake mtaalamu wa ufatiliaji na tathmini kutoka TAMWA-ZNZ Muhammed Khatib amesma baadhi ya wananchi wamekuwa hawana uwelewa wa kutosha kuripoti na kufuatilia kesi za udhalilishaji wanazofanyiwa hivyo ni vyema waandishi kuweza kutumia kalamu zao kwa kuelimisha jamii ili iweze kuwa salama na kupungua kwa vitendo vya udhalilishaji.
Akiwasilisha mada inayohusu udhlilishsji katika sekta ya kilimo na biashara Mjumbe wa Bodi TAMWA-ZNZ Haura Shamte amesma ni vyema waandishi wa habari kufika maeno ya mashamba kwani tathmini zinaonesha kuwa maeneo ya vijiJIni kuna ongezeko kubwa la vitendo vya udhalilishaji hususani wanawake wanapoingia katika shughuli zao za kilimo., ikiwemo kupewa mgawanyo mdogo wa fedha baada ya mavuno.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo ni chchu ya kuongeza uchechemuzi kwa haki za wanawake na wasichana na wameahidi kuyafanyia kazi na kuweza kutoa elimu iliyo kwa jamii ili kuweza kubaki salama na kupunguza vitendo vya udhalilishaji kwa makundi hayo.
Mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha miezi minane katika mikoa miwilii ikiwemo mkoa wa Kaskazini Pemba na Kaskazini Unguja na unatarajiwa kuwafikia watu zaidi ya elfu 50 ndani ya mikoa hiyo. Kauli mbiu ni FAMILIA SALAMA JAMII SALAMA, JAMII SALAMA FAMILIA SALAMA.




No comments