Minara 372 Kuleta Mageuzi Huduma Ya Umeme Zanzibar.
Na Siti Ali.
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Mhandisi Haji Mohamed Haji, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea na jitihada za kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme wa uhakika kwa wananchi.
Mhandisi Haji ameyasema hayo leo, Oktoba 28, 2026, wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua vituo vya kupokea na kusambaza umeme vilivyopo Makunduchi, Zanzibar.
Amesema Serikali imesaini makubaliano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uzalishaji na usambazaji wa umeme visiwani Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme ya uhakika inayokidhi mahitaji yao.
Aidha, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikitumia fedha za ndani kugharamia utekelezaji wa miradi ya umeme ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati, ikiwemo miradi inayohusisha matumizi ya nishati ya jua.
sambamba na hayo ameeleza kuwa juhudi hizo zina lengo la kuimarisha miundombinu ya umeme, kuongeza upatikanaji wa nishati na kuboresha huduma kwa wananchi pamoja na shughuli za kiuchumi visiwani Zanzibar.


.jpeg)
very good
ReplyDelete