WANANCHI WAHIMIZWA KUHIFADHI MAZINGIRA.
NA NISHAN KHAMIS
Mbunge wa Jimbo la Chaani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahmoud, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi wa mazingira.
Ameyasema hayo katika kikao na Kikundi cha Kuhifadhi Mazingira cha Kikobweni, ambapo Ayoub amesema wananchi wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kulinda mazingira kwa kufanya usafi, kupanda miti, kuepuka utupaji holela wa taka pamoja na kushirikiana na mamlaka katika kutatua changamoto zinazohusiana na mazingira.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Jimbo la Chaani, Juma Usonge Hamad, amesema viongozi wa jimbo hilo wataendelea kuunga mkono juhudi za wananchi na vikundi mbalimbali vinavyotekeleza shughuli za maendeleo.
Amesema dhamira ya viongozi wa Jimbo la Chaani ni kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi katika kila sekta, ikiwemo mazingira, afya, elimu, maji na huduma nyingine muhimu kwa jamii.
Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha Kuhifadhi Mazingira, Msikitu Juma Haji, ametoa pongezi kwa viongozi hao kwa kuendelea kusikiliza changamoto za vikundi na kutoa ushirikiano katika shughuli za uhifadhi wa mazingira.
Amesema msaada huo utasaidia kikundi kuongeza ufanisi katika kazi zake na kuwataka viongozi kuendelea kuwa karibu na vikundi vya wananchi ili kuimarisha juhudi za pamoja katika kulinda


No comments