KAMATI YA WATAALAMU WA VYOMBO VYA HABARI ZANZIBAR (ZAMECO) YATAFAKARI MAFANIKIO YA NUSU MWAKA, YACHAGUA VIONGOZI WAPYA
Na Safia Mohamed.
Kamati ya Wataalamu wa Vyombo vya Habari Zanzibar (ZAMECO) imefanya kikao chake cha nusu mwaka kilicholenga kutathmini utekelezaji wa shughuli zake kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2026, kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza, pamoja na kuweka mikakati ya kuimarisha sekta ya habari Zanzibar.
Katika kikao hicho, wajumbe walieleza kuridhishwa na hatua zilizopigwa katika kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari unaozingatia maadili, weledi na uwajibikaji. Pia walitambua mchango wa ZAMECO katika kuendeleza sauti ya pamoja ya wadau wa habari kwenye mijadala ya sera na marekebisho ya sheria zinazohusu sekta ya habari Zanzibar.
Kamati ilisisitiza kuwa itaendelea kushiriki kikamilifu katika juhudi za kutetea uhuru wa vyombo vya habari, kulinda haki ya kujieleza, na kuimarisha uwajibikaji katika sekta ya habari kwa manufaa ya jamii na maendeleo ya kidemokrasia.

Katika kujadili mwelekeo wa kipindi kijacho, wajumbe walikubaliana kuimarisha utendaji wa kamati kupitia utekelezaji wa mikakati endelevu itakayosaidia kukuza sekta ya habari. Miongoni mwa vipaumbele vilivyowekwa ni kuongeza wanachama ili kuwafikia wadau wengi zaidi, kuendelea kutetea mazingira bora ya kisheria yanayounga mkono uhuru wa habari, pamoja na kuhakikisha ulinzi na usalama wa wanahabari na watetezi wa haki za binadamu.
Aidha, kikao kilipendekeza kuanzishwa kwa kamati ndogo za kitaalamu zitakazosaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za ZAMECO, ikiwemo kufanya tafiti, kutoa mafunzo, kufanya utetezi na kufuatilia masuala yanayoathiri mazingira ya kazi za vyombo vya habari na nafasi ya kiraia nchini.
Katika hatua nyingine, wajumbe walifanya uchaguzi wa viongozi rasmi wa kamati ambapo Abdallah Mfaume alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Dkt. Mzuri Issa kuwa Makamu Mwenyekiti, na Zaina Mzee kuwa Katibu Mkuu wa ZAMECO.
Viongozi hao wanatarajiwa kuiongoza kamati katika kuendeleza dhamira yake ya kuimarisha taaluma ya habari, kukuza ushirikiano kati ya wadau wa sekta ya habari na kuendelea kutetea uhuru wa vyombo vya habari Zanzibar.
ZAMECO ni jukwaa linalowakutanisha waandishi wa habari wakongwe kutoka vyombo vya habari vya serikali na binafsi, likiwa na lengo la kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari, kulinda uhuru wa habari na kuchochea uwajibikaji katika jamii. Kamati inaongozwa kwa ushirikiano wa taasisi mbalimbali za habari na haki za binadamu, zikiwemo Media Council of Tanzania (Zanzibar), Zanzibar Press Club (ZPC), Journalists for Development Association (WAHAMAZA), Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) na Tanzania Media Women's Association – Zanzibar (TAMWA ZNZ).
Kupitia ushirikiano huu, ZAMECO inaendelea kujijengea nafasi kama jukwaa muhimu la wadau wa habari linalochangia kulinda uhuru wa vyombo vya habari, kukuza taaluma ya uandishi wa habari na kuimarisha misingi ya uwazi, uwajibikaji na utawala bora Zanzibar.

great
ReplyDelete