Breaking News

MAZUNGUMZO SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA YANAENDELEA , DKT MWINYI.



Na Siti Ali.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema mazungumzo ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kati ya CCM na ACT-Wazalendo yanaendelea, huku akisisitiza kuwa CCM itaendelea kusimamia maslahi ya Taifa na Chama kwa ujumla.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika mkutano wa kutoa shukrani baada ya Uchaguzi Mkuu, hafla iliyofanyika Mahonda, ambapo amewataka viongozi na wanachama wa CCM kujitathmini, kuimarisha umoja na kujipanga mapema kuelekea Uchaguzi wa mwaka 2030.



Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha maadili, utekelezaji wa Ilani, uchumi wa Chama pamoja na kudumisha amani, huku akieleza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha uchumi kupitia miradi ya maendeleo, maboresho ya bandari na juhudi za upatikanaji wa umeme mbadala. 



No comments