Breaking News

ZIDO YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 30 KWA WATU WENYE ULEMAVU .



 Na Safia Mohammed.

Taasisi ya Zanzibar International Development Organization (ZIDO) imesema itaendelea na juhudi za kukuza na kuimarisha ustawi wa wananchi hasa watoto yatima na makundi ya watu wenye ulemavu nchini.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo  Ramadhan Makame Mbanja  ameseyasema hayo  huko Dunga wakati akikabidhi vitu mbalimbali kwa watoto yatima, watu wenye ulamavu wa viungo pamoja na ngozi.

Amesema Taasisi hiyo imekuwa ikitoa msaada wa karibu kwa makundi hayo kwa kuyasaidia mahitaji na huduma mbalimbali ili kuhakikisha na wao wanajiona sawa na watu wengine katika jamii na wanastahili kupata haki zote za msingi.



Amesema vifaa hivyo vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni thalathini vitawarahisishia katika shughuli zao za kiuchumi, kielimu na kimaisha. 

Afisa ulemavu Wilaya ya Kati ndugu Abdalla Aladi amesema utolewaji wa vifaa hivyo kwa watu wa makundi ya watu wenye ulemavu unatoa faraja na furaha kwani huweza kutimiza ndoto zao za maisha.

Aidha amewahimiza wazazi wenye watoto wenye ulemavu kutowaficha majumbani na badala yake kwenda kuwaorodhesha wilayani ili waweze kutambulika na kupatiwa haki zao za msingi.



Katibu wa Taasisi ya watu wenye ualbino Zanzibar  Mohd Ali Mohd na  wananchi waliopatiwa msaada huo  Mwanakombo Mohammed na bwana Ali Mzee wameelezea kufurahishwa kwao na misaada hiyo waliopatiwa kwani  itawarahisishia shughuli zao ikiwemo za malezi pamoja na kujiwezesha kiuchumi.

Msaada uliotolewa na Jumuiya hiyo ni pamoja na vifaa vya skuli kwa watoto yatima 40, visaidizi mwendo 40 kwa watoto wenye ulemavu wa viungo na mbuzi 100 kwa familia kumi na tano kwa ajili ya kufuga, ambavyo vimegharimu jumla ya shilingi milioni thalathini




  

No comments