SERIKALI KUENDELEZA MIUNDOMBINU NCHINI.
Na Siti Ali.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaongeza kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, hususan ujenzi wa miundombinu na barabara za kisasa, ili kuibadilisha nchi kuwa ya kisasa. Aidha, amesema Serikali itaendelea kuimarisha maslahi ya wafanyakazi, wastaafu na wazee kadri hali ya uchumi itakaporuhusu.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Mjini Kichama katika mkutano maalum wa kutoa shukrani baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 hafla iliyofanyika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Amani.
Katika mkutano huo, Dkt. Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kudumisha umoja ndani ya CCM kwa kuvunja makundi baada ya uchaguzi kumalizika, huku akiwataka wabunge, wawakilishi na madiwani kuwaunganisha wanachama.
Amesema pia Chama kinapaswa kuwa na uchumi imara kupitia miradi mikubwa ya kisasa ili kujiendesha kwa ufanisi



No comments