Breaking News

ZAFIRI YAKABIDHIWA MUUNDO WA TAASISI KUIMARISHA UTENDAJI KAZI .




Na Said Khamis.

Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini Zanzibar ZAFIRI imepokea Muundo wa Taasisi kutoka Kamisheni ya Utumishi wa Umma kwa lengo la kuimarisha utendaji wa kazi, ufanisi na uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo.

‎Akikabidhi muundo huo Katibu kamisheni ya Utumishi wa Umma Kubingwa  Mashaka Simba huko ofisini Mwanakwereke Amesisistiza kuwa miundo hiyo ni nyenzo muhimu ambayo inaboresha utendaji wa kazi na kuimarisha utowaji wa huduma kwa jamii 



‎Amesema kuwa kamisheni ipo tayari mda wowote kushirikiana katika kutowa ufafanuzi wa kitaalamu pale unapohitajika ili kuhakikisha muundo huo unatekelezwa kwa ufanisi na kuleta mabadiliko chanya.

‎Nae Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini Zanzibar ZAFIRI Dkt. Zakaria Ali Khamis ametowa Shukurani kwa Kamisheni ya Utumishi wa Umma kwa mashirikiano mazuri yaliowezesha kukamilika kwa muundo huo.



‎Aidha amesema Muundo huo  utaimarisha kuweka uwazi wa majukumu ya Taasisi katika utendaji kazi, ufanisi, utekelezaji, mafanikio, changamoto, na uboreshaji wa kazi za kitafiti za uvuvi  na  Maliasili za baharini kwa maendeleo ya Jamii na Nchi.


No comments