S

Katika dimba la Prince Moulay Abdellah, Rabat,macho ya mashabiki wa Afrika Mashariki na wengine yataelekezwa kwenye pambano la Raundi ya 16 ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 kati ya wenyeji Morocco na Tanzania. Ni mechi inayokutanisha timu mbili zenye hadithi mbili tofauti kabisa: moja ikiwa na historia, ubora na matarajio ya ubingwa, nyingine ikiwa katika safari ya kihistoria na ndoto ya kuandika ukurasa mpya wa soka lake.

Morocco wanaingia wakiwa wababe wakubwa, wakibebwa na ubora wa kikosi, uzoefu wa mashindano makubwa na nguvu ya kucheza nyumbani. Lakini licha ya kupewa nafasi kubwa ya ushindi, kocha Walid Regragui amesisitiza jambo moja muhimu: unyenyekevu, na kuiheshimu Tanzania. AFCON mara nyingi imewafundisha vigogo kuwa jina peke yake halitoshi.

Kwa Tanzania, huu ni mtihani mkubwa zaidi kuwahi kuikabili Taifa Stars katika historia ya AFCON. Kufuzu kwa mara ya kwanza hatua ya 16 bora tayari ni mafanikio, lakini wachezaji na benchi la ufundi wanasisitiza hawapo Morocco kwa matembezi. Wanaingia bila presha, wakiwa na kiu ya kushangaza Afrika.

Katika mazingira hayo, huu si tu mchezo wa soka, bali ni pambano la kisaikolojia na kihistoria, uzoefu dhidi ya ndoto, na ubora dhidi ya ujasiri.

s

Chanzo cha picha,


Maelezo ya picha,

Kwa takwimu na historia, Morocco inaingia uwanjani ikiwa juu kwa kila kipimo. Katika mechi 8 zilizopita walizokutana awali kati ya timu hizi katika mashindano yote, Morocco imeshinda 7, huku Tanzania ikishinda mara 1 tu ushindi wa kihistoria wa mabao 3-1 mwaka 2013 katika kufuzu kombe la dunia. Mbwana Samatta ambaye miaka 13 baadaye anakuja kukutana na tena alifunga mawili, Thomas Ulimwengu alifunga moja. timu hizi hazikuwahi kuwa na sare katika mechi hizo.

Katika mechi 5 za mwisho mfululizo, Morocco ameibuka mshindi bila hata kuruhusu bao. Tanzania imeshindwa kufunga katika mechi 4 za mwisho dhidi ya Atlas Lions. Kwenye AFCON 2023, Morocco waliwafunga Taifa Stars 3-0 hatua ya makundi, na kwenye CHAN 2024 waliwatoa wenyeji Tanzania kwa ushindi wa 1–0 wakaenda kutwaa ubingwa.

Morocco pia ina historia kubwa barani Afrika, imetwaa ubingwa wa AFCON mara 1 mwaka 1976, imefika fainali, nusu fainali mara kadhaa, na kwa sasa ni namba 1 Afrika na namba kwa ubora wa soka na namba 11 duniani kwa viwango vya FIFA.

Tanzania, kwa upande mwingine, ipo namba 112 duniani na 22 Afrika, na bado haijawahi kushinda mechi yoyote kwenye fainali za AFCON. Mbali na hivyo matokeo yao ujumla katika mechi walizocheza na mataifa mbalimbali katika miezi mitatu iliyopita, tofauti ni kubwa: Morocco katika mechi 7 zilizopita haijafungwa hata moja, imeshinda 6, na sare 1, wakiruhusu bao 1 pekee dhidi ya Mali walipokwenda sare ya 1-1 mwezi uliopita kwenye AFCON 2025.

Skip Iliyosomwa zaidi and continue reading

End of IliyosomwaTanzania katika mechi 7 zilizopita haijashinda hata moja, imefungwa 5, sare 2 za juzi dhidi ya Uganda na Tunisia, ikiwa na mabao 6 ya kufunga na 11 ya kufungwaKwa mantiki hiyo, historia na takwimu zinaihukumu Tanzania mapema kabla hata kipyenga hakijapulizwa. Lakini ndoto zao huenda zikawapendelea.