Breaking News

WANANCHI WAHIMIZWA KUPANDA MITI KUTUNZA MAZINGIRA

 Na Mwandishi wetu.

Wananchi wa Kata ya Isakalilo wameshauriwa kuwa na utamaduni wa upandaji wa miti ili kukabiliana na  mabadiliko ya tabia nchi Pamoja na urejeshwaji wa uoto wa asili uliopotea katika mazingira yanayowazunguka.

Hayo yamesemwa na Daniel Kalinga ambaye ni Mkurugenzi wa Shule ya Awali na Msingi KALDAN, iliyoko katika kata ya Isikalilo mtaa wa Kitasengwa ndani ya manispaa ya Iringa alipokuwa anazungumza na wananchi wanaoishi karibu na shule mara baada ya kukabidhi miti ya matunda ya Mparachichi kwa kila mmoja.

Kalinga amesema kuwa wananchi hawana budi kuendelea na utunzaji wa misitu Pamoja na upandaji wa miti na kwa mazingira ya Kitasengwa yamezungukwa na miti hivyo hatuna budi kuanza kupanda miti ya matunda licha ya kusaidia utunzaji wa mazingira ila ni chanzo kizuri cha mapato kwa mwananchi.

Aidha amesema kuwa  upandaji wa miti wananchi wanaweza kupanda miti yenye manufaa ikiwemo ya matunda  kama vile miembe,,mipapai , mpera na miti mingine ya matunda ambayo inaweza kuwa sehemu ya kilimo na wakati mwingine ikitunza mazingira .

Akizungumzia mikakati ya shule hiyo mazingira eneo la Kitasengwa katika utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti amesema kuwa wanaendelea na uboreshaji na  utaratibu wa kuwa na klabu za wanafunzi mashuleni ili baadae wawe  msaada mkubwa wa kuelimisha jamii  juu ya utunzaji wa Mazingira.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi afisa walimshukuru Mkurugenzi Daniel Kalinga kwa kuonyesha moyo wa Kutunza mazingira na kuwapatia miti ya Mparachichi kwani licha ya kuwa faida kwao ila itasaidia kutunza mazingira.

Mmoja ya wananchi walipokea miti hiyo Daniela Mtanda ameelezea umuhimu wa uwepo wa miti na misitu katika Maisha ya binadamu kuwa ni Pamoja na upatikanaji wa dawa ,vyakula Pamoja na kusaidia kuzuia mmonyoko wa udongo.


No comments