ZFDA YAISHIKILIA MINOFU ILIYOPITWA NA MUDA ZAIDI YA KILO1,2OO,

NA FATMA RAJAB
Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA), inashikilia kilo 1,232.64 za bidhaa za nyama iliyopitwa na muda, walioibaini kwenye moja ya chumba cha kuhifadhia baridi cha kampuni ya JM Investiment iliopo Fuoni Ijitimai.
“Miongoni mwa kilo hizo vipo vipapatiro boksi 55 sawa na kilo 660 kutoka Dubai, kuku chiken naget kutoka Uturuki paketi 254 sawa na kilo 103.4, kuku kidari paketi 58 sawa na kilo 34 na nyama ya ngombe paketi 12 sawa na kilo 15.24.” alisema Mkaguzi wa Chakula Dk. Thamra Khamis Talib wakatia akizungumza na waandishi wa habari kufuatia tukio hilo.
Alieleza kuwa wakati maofisa wa ZFDA wakifanya ukaguzi wao wa kawaida waligundua bidhaa hiyo ikiwa imehifadhiwa huku ikiwa Katika vifungashio visivyo vya asili na kubadillishwa mwisho wa tareh ya matumizi jambo ambalo ni kosa kisheria.

Alibainisha kuwa kutokana na kuwa bidhaa hiyo sio salama kwa matumizi ya binaadamu itaendelea kuwa chini ya ZFDA hadi pale mmiliki atakapokamilisha taratibu za uteketetezaji kwa lengo la kumlinda mtumiaji.” Tumeona kama hivi vipapatiro vinavyotoka Dubai kilo 420 vimebadilishwa vifungashio na taarifa zake na baadhi ya bidhaa nyengine zimebadilika rangi ya asili, hii inaashiria kuwa bidhaa hizi hazifai kwa matumizi ya binadamu ni lazima tukaziteketeze na tumemtaka mfanyabiashara kuja ofisini kwa taratibu za uteketezaji kwa gharama zake naa adhabu nyengine zitafuata Kwa mujibu wa sheia ya ZFDA,” Alisema Thamrat.
Alitumia fursa hiyo kuwasisitiza wafanyabiashara wengine kuwa wazalendo na kuendelea kushirikiana na ZFDA katika kumlinda mtumiaji na kubainisha kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa atakaekwenda kinyume.
Mapema alieleza kuwa ZFDA itaendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuhakikisha wanakua na uelewa wa kutosha juu ya masuala hayo na wanashiriki kikamilifu kuwafichua wafanyabiashara kama hao.

Akizungumza kwa niaba ya JM Investiment mmoja wa watendaji wa kampuni hiyo ambae jina lake limehifadhiwa alisema wao walinunua kontena pekee na bidhaa iliyokuwemo ndani yake ilikusudiwa kuangamizwa.
Aidha alieleza kuwa waliendelea kuhifadhi bidhaa hiyo si kwa matumizi ya binaadamu lakini walitumia kidogo kidogo kulisha mbwa watatu waliopo katika kampuni hiyo ambopo alieleza kuwa hawakuwa walijua kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.” Sisi tulikua hatuuzi nyama hii ilikua tunawalisha mbwa wetu watatu wale pale, kosa letu ni kuwa hatukuwajuulisha ZFDA kuwa tumehifadhi hii bidhaa kwa ajili ya Chakula cha wanyama na kuahidi hawatorejea tena.” Alisema mtendaji huyo.
No comments