WADAU WA BIASHARA YA DAGAA ZANZIBAR WAHIMIZWA KUZINGATIA MUONGOZO WA SERIKALI.
Na Said Khamis.
Wadau mbali mbali wa Biashara ya Dagaa Zanzibar wametakiwa kufuata taratibu na muongozo ulioekwa na Serikali ili kuondoa changamoto mbali mbali zinazojitokeza kwenye mnyororo mzima wa Biashara ya Dagaa hapa nchini.
Amesema hayo Mkuu wa Divisheni ya Usarifu wa Mazao ya baharini Zanzibar Nd. Ali Khamis Shafi kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi wakati wa kuendesha kikao cha Kamati ya Muongozo wa Dagaa huko Maruhubi Unguja.
Mkuu huyo amesema kuwepo kwa muongozo wa biashara ya Dagaa kutasaidia kuondoa changamoto ya bei isiokuwa rasmi inayofanywa na Wavuvi na Waanikaji dagaa jambo ambalo limekua tatizo kwa wanunuzi na wasafirishaji wa Dagaa nje ya nchi.
Sambamba na hilo ametoa wito kwa Wadau hao kuwa walimu kwa wengine kwani kufanya hivyo kutapelekea kupatikana takwimu sahihi za usafirishaji wa dagaa nje ya nchi na kuongeza pato la Serikali.
Hata hivyo ametoa msisitizo kwa Wavuvi kuuza madagaa katika Madiko yanayokubalika kisheria ili kuondosha changamoto ya bei kwa Waendesha biashara hiyo.
Nae Mwenyekiti wa Uwadaza Nd. Haji Haji amesema muongozo wa dagaa kwa upande wa Zanzibar utasaidia sana kuondoa matatizo mbali mbali yanayojitokeza katika biasahara hiyo kwa maslahi ya ndani na nje ya Zanzibar.
Nao Washiriki wa Kikao hicho wamesema wapo tayari kutoa elimu kwa wengine ili kuondosha changamoto mbali mbali zinazojitokeza wakati wa ufanyaji wa biashara hiyo.
Kikao hicho cha siku kichofadhiliwa na Idara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mazao ya Baharini Zanzibar kwa kushirikiana na Umoja wa Waanikaji wa Madagaa Zanzibar na kuwashirikisha Waanikaji ,Maajent na Wasafishaji wa Dagaa.
.jpeg)

No comments