Breaking News

ZOP YAFANYA UCHUNGUZI NA MATIBABU ya MASIKIO KWA VIZIWI.

 


Na Siti Ali.

Taasisi inayosaidia jamii Zanzibar (ZOP)imefanya zoezi la uchunguzi na matibabu bure ya masikio kwa watoto wenye ulemavu wa masikio (VIZIWI)kwa lengo la kujua afya zao.

Akizungumza katika zoezi hilo lililofafanyika huko katika skuli ya viziwi iliyopo kiembe samaki Katibu wa taasisi hiyo Daktari Naufal Kassim Muhammed amesema kuwa lengo la kutoa matibabu hayo ni kuwasaidia wanajamii kwa kuwapa matibabu bure pamoja na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuyatunza masikio ili kujiepusha na uziwi wa kudumu.

Aidha Daktar Naufal ameelezea sababu mbali mbali zinazochangia kupata maradhi haya ya uziwi ikiwa ni pamoja na kula vyakula vya makopo pamoja na kutumia earphone kwa jambo ambalo limekuwa likitumika sana kwa vijana,kusafisha masikio kiholela na mengineyo.

“Sababu zinazochangia kupata maradhi ya uziwi ni pamoja na kula vyakula vya makopo pamoja na kutumia earphone kwa jambo ambalo limekuwa likitumika sana kwa vijana,kusafisha masikio kiholela, kuingiza dawa za kienyeji kama vile mafuta ya nazi,kutia vitunguu thaumu kutumia vyenye sukari nyingi na mengineyo” ameeleza Daktari Naufal.

Sambamba na hayo amesema kuwa jamii haina muamko wa kuwatunza watoto viziwi kwani wamekuwa wakiwabagua jambo ambalo hupelekea unyanyasaji,na kuwaomba wazee wenye watoto viziwi kutokuwafungia ndani na badala yake kuwatoa ili kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu kwani na wao ni watoto kama watoto wengine.

Nao wazee wa watoto viziwi waliofika katika matibabu hayo wameishukuru taasisi ya ZOP kwa kuwapatia elimu na matibabu na kuahidi kuifanyia kazi pamoja na kuwa mabalozi wazuri kwa wengine na kuiomba taasisi hiyo kuendelea kuisadia jamii ili kupata ujira mbele ya Allah (SW).

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi hiyo Walid Kassim Muhammed amesema kuwa katika taasisi yao wamekuwa wakisaidia sana jamii hususani kwa watoto wenye ulemavu wa uziwi kwa kueka skuli maalumu inayowasomesha viziwi matamshi na sauti ili waweze kuwasiliana na jamii inayowazunguka



No comments