WAZAZI NA WALEZI WAPEWA SOMO, MALEZI BORA YA WATOTO
Wzazi na waleziwa wametakiwa kuwalea watoto wao katika madili yaliokuwa Bora ili kuepukana na changamoto mbali mbali ambazo zinaweza kujitkeza kwa watoto hususani katika kipndi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa zaznibar.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Siti Abas Ali katika mafunzo ya kutoa elimu ya malezi kwa waratibu kutoka shehia zote za Unguja pamoja na wazazi na walezi kuhusiana malezi hafla iliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa skuli ya sekondri Tumekuja.
Amesema lengo la kuanzishwa kwa mafunzo Hayo ni kuweza kusimamia malezi na tamaduni za kizanzibari, ''ni lazima watoto walindwe wasimamiwe wapatiwe elimu iliyobora ili kuweza kupata viongozi waliokuwa bora wa baadae kwani vijana ndio Taifa la kesho'' ameeleza Mkurugenzi Siti
Aidha amewakumbusha wazazi na walezi kuzungumza na vijana wao wajiepushe na kukaa na watu wanaofanya uvunjifu wa amani hususani katika kipindi hichi cha uchaguzi, kwani amani ikivunjika waathirika wakubwa ni wanawake na watoto.sambamba na hilo amewataka wazazi na walezi kutowahusisha watoto na vyama vya kisiasa ili kuepusha changamoto mbali mbali zinaweza kujitokeza kwa jamii.
Nae meneja wa mradi wa mafunzo ya malezi ya kinababa na kinamama katika Jumuiya ya Vijana elimu Maendeleo ya Mazingira Zanzibar ( ZAYADESA ) Aisha Ali Amani Karume Amesema kuwa lengo la mafunzo Hayo ni wawezesha wazazi namna ya kuwalea watoto katika mazingira bora na kuwakinga kuingia katika makundi hatarishi. Pamoja na kuelewa changamoto mbali mbali ambazo wanakabiliana nazo.
Kwa upande wao wazazi na walezi waliopatiwa mafunzo hayo wamesema mafunzo Hayo yamewasaidia kujua jinsia Gani wanaweza kuwalea watoto wao wa kike na wakiume kirafiki ili kuweza kuwafikishia matatizo yao na changamoto na kujua ni jinsi Gani wanaweza kuzitatua changamoto hizo.
Mafunzo Hayo yameandaliwa na taasisis ya ZAYADESA kwa kushirikian na mama shadiya karume ya kutoka elimu kwa wazazi wa kike na wakiume na mafunzo Hayo yamechukuwa takribani wiki kumi kwa kuwakutanisha wazazi na walezi katika wilaya zote za Unguja
No comments