Breaking News

WAKULIMA WILAYA YA KATI WASHAURIWA KUTUMIA MBINU ZA KISASA

 


SAID KHAMIS WILAYA YA KATI.

Wakulima wa mazao ya mboga mboga nchini wameomba  kupatiwa elimu ya kilimo kmara kwa mara na wataalamu ili waweze kulima kilimo cha kisasa na kuacha tabia ya kulima kimazoea.

Wakizungumza na TOZ wakulima mbalimbali kutoka wilaya ya kati wamesema elimu ndogo ya kuchagua mbegu bora inayostahamili na ukame na kutoa mavuno mengi huwafanya kukosa kupata mavuno bora katika kilimo chao ambacho wanakitegemea katika kuwapatia riziki zao za ila siku.

‘’Wakulima wengi baadhi yetu hatulimi kwa kufuata ushauri wa wataalamu tunalima tu ili mradi tupate riziki ya kula na watoto ikitokea mazao yamekua mengi ndio tunauza kwa ajili ya kupata kipato’’ walisema wakulima.

Sambamba na hayo wakulima hao waliwashauri wakulima wenzao kuzitumia  vizuri mvua za vuli kwa kufuata ushauri wa wataalamu, ambapo mvua hizo zimeanza kunyesha mwezi Oktoba na zinatarajiwa kunyesha hadi Disemba mwaka huu.



Wakulima wa mazao ya chakula ikwemo mboga mboga, nafaka pamoja na mazao ya mizizi wametakiwa kutokulima katika maeneo yanayotuwama maji kwa muda mrefu ili kupata mavuno mazuri ya mazao waliyoyapanda.

Akizungumza na TOZ Afisa Mazao ya Chakula wilaya ya kati Zamani Omar Abeid amesema, kuelekea msimu wa mvua za vuli wakulima wanatakiwa kulima sehemu za juu zisizo tuwama maji zaidi ya siku mbili ili kuepusha mazao kuharibika.

Afisa huyo amesema mazao ya mbogamboga ikiwemo tungule na matikiti maji hayawezi kusatahamili maji muda mrefu. Aidha amesisitiza kuwa wakulima wanaolima maeneo ya juu kuendelea na kilimo hicho.

‘’kuna baadhi ya maeneo ya kilimo yanatuwama maji kwa muda mrefu Zaidi ya siku mbili kwahiyo maeneo hayo inapofika kipindi cha mvua si rafiki kwa kufanya shughuli za kilimo ikiwa unategemea kupata mazao’’ amesema Afisa huyo.

Hata hiyo amewashauri wakulima kufuata ushauri wa waataalamu wa kilimo kabla ya kuandaa mashamba yao kwani wakuilima wengi wamezoa kulima kimazoea bila kufahamu ni aina gani ya mazao yanatakiwa kupandwa katika msimu husika.

Mvua za vuli ni miongoni mwa mvua zinazotegemewa sana na wakulima kupanda mazao yao ingawa zimeathiriwa na mabadiliko tabianchi



No comments