Breaking News

KURA 414 ZATHIBITISHA KUWA MWANAMKE ANAWEZA KUWA KIONGOZI

 


Na Thuwaiba Habibu, Zanzibar.

"Nilishindwa kwa kura mbili tu, lakini nimeandika ushindi mkubwa katika mioyo ya wengi"

Katika uchaguzi wa uwakilishi uliofanyika katika Jimbo la Bububu, jina la Tatu Hussein Abdallah limebaki midomoni mwa watu wengi. Licha ya kupata kura 414 na kupitwa kwa kura mbili tu na mpinzani wake  Waziri  wa utalii Mudrik Ramadhani soraga aliyepata 416, safari yake ya kisiasa imeibua msisimko mpya kuhusu nafasi ya mwanamke katika uongozi.

Kwa wengine, matokeo haya yangekuwa sababu ya kuvunjika moyo. Lakini kwa Tatu, yalikuwa ni ushindi mkubwa wa heshima, matumaini, na uthibitisho kuwa wanawake wana uwezo mkubwa wa kuongoza jamii zao kama watapewa nafasi.

Safari ya Maisha na Elimu

Tatu Hussein Abdallah alizaliwa mwaka 1984 katika kijiji cha Kizimbani eneo la Sakafuni Wilaya ya Magharib "A".  Kwa sasa ana umri wa miaka (41)Ni  mama wa watoto wanne. Elimu yake ya awali aliipata katika Skuli ya Msingi ya Langoni na baadaye kujiunga na Skuli ya Kidongo Chekundu mwaka 2000. Aliendelea na masomo hadi kufikia shahada ya Uzamivu katika fani ya  Rasilimali Watu na Uongozi  (Master) katika Chuo kikuu cha Zanzibar ( ZU) hatua kubwa inayoonesha dhamira yake ya kweli katika kuleta mabadiliko chanya kwa jamii.

 

Uzoefu na Uwanachama wa Kisiasa

Tatu ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tangu akiwa kijana, na alihudumu katika  shehia 31  ndani ya majimbo 5 tofauti. Uzoefu huu aliupata  ulimwezesha kujenga ujasiri wa kugombea kwa mara ya kwanza nafasi ya Uwakilishi, akiwa na maono na mkakati wa kusaidia jamii yake.

Cheo chake katika serikali

Cheo chake kwa sasa katika serikali ni  Mkuu wa Idara  huduma za jamii,mazingira  na mipango miji.

 Pia alikuwa  Kaimu Mkurugenzi  wa Manispaa ya Magharib"A"

Vile vile  katibu  wa Jumuiya  ya Rafiki Wanawake na Watoto Zanzibar (RAWAZA).

 

 

Sababu ya Kugombea

Kilichomsukuma kugombea ni mapenzi yake kwa Jimbo la Bububu, eneo alikozaliwa, analolifahamu kiundani Aliona ni wakati muafaka wa kusimama kama sauti ya watu, hasa vijana na wanawake, na kuibua changamoto zinazowakabili.

 

"Niliona vijana wanakabiliwa na tatizo la ajira, nikaamua kuweka mikakati ya kuwawezesha kujiari, badala ya kusubiri tu kuajiriwa na serikali," amesema Tatu.

Pia alilenga kuwajengea uwezo wanawake kupitia mafunzo ya uongozi na kuwaelimisha kwamba kuwa Uongozi si heshima ya wachache, bali ni haki ya kila mtu bila kujali jinsia.

 

Changamoto na Mafanikio

Changamoto kubwa aliyokutana nayo ilikuwa kubezwa kwa sababu ya jinsia yake.

"Wengi walinibeza kwa sababu mimi ni mwanamke, lakini sikuvunjika moyo. Niliamini katika uwezo wangu na nikasimama kidete kugombea," amesema kwa msisitizo.

Lakini ndani ya changamoto hizo, alipata mafanikio makubwa. Mwanamke huyu jasiri aliweza kuwashinda wanaume 2 katika awamu ya pili ya uchaguzi,ambako kulikuwa na jumla ya watu 4 jambo lililoashiria imani kubwa ya wananchi wa jimbo hilo.

Wanawake wengi walijitokeza kumpigia kura, wakiona kuwa anaweza kuwa kiongozi mwaminifu na mwenye dira.

Aidha, familia yake ambayo mwanzoni haikuamini uwezo wake, ilikuja kumuunga mkono kwa dhati baada ya kuona azma yake ya kweli ya kuleta mabadiliko.

 

Ushauri kwa Wanawake

"Wanawake wanatakiwa wajiamini. Kila kitu kinawezekana kama utakapojitolea  na kuweka jitihada. Uongozi ni haki ya kila mmoja wetu."

Hata hivyo ameonesha kuwa hata bila ushindi wa nafasi ya kwanza, ameshinda vita kubwa ile ya kuibuka kama sauti ya wanawake, mfano wa kuigwa, na kielelezo cha mabadiliko ya kweli katika jamii.

"Hili ni mwanzo tu si mwisho wa safari. Nitajitokeza tena kwa nguvu zaidi, kwa sababu sauti ya mwanamke sasa haisikiki tu, bali inasikika na kufahamika na wengi



No comments