WAZIRI SHAABAN ATOA WITO WA MASHIRIKIANO ILI KUKUZA AJIRA ZA VIJANA ZANZIBAR
Na Fatma Rajab 24/11/2025.
Waziri wa Vijana Ajira na Uwezeshaji Mhe. Shaaban Ali Othman amewataka watendaji wa Wizara hiyo Kuendeleza mashirikiano pamoja na kubadilika kiutendaji ili kuakisi matakwa ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi ya kuwapatia Vijana Ajira Nchini.
Akizungumza na viongozi pamoja na wafanyakazi katika hafla ya ukaribisho wa Ofisi katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Vijana Migombani, Wilaya ya Mjini.
Amesema ni wajibu wa kila mfanyakazi kufuata muongozo wa ilani ili kufanikisha malengo ya Serikali sambamba na ushirikiano katika uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya Kazi zao.
Aidha amesema kuwa mwanga wa Matumaini ni mashirikiano ya pamoja ambayo ni nguzo muhimu ya kufanikisha malengo na majukumu Kwa ufanisi mkubwa bila ya kutoka nje ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Nae Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe Hassan Khamis Hafidh amesema Timu iliyopagwa katika Wizara hiyo ni Timu sahihi hivyo watahakikisha wanatekeleza azma ya Serikali kuhakikisha Vijana wanafikia ndoto zao .
Amesema Vijana ndio tegemeo la Taifa lolote Duniani na ndio nguvu Kazi ya Taifa tunasikitishwa kwa baadhi ya watu utayari wao wa kufanyakazi bado ni mdogo
Nae Katibu Mkuu Salama Mbarouk Khatib amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi kwa kuwaamini na kuahidi kusimamia vyema majukumu yao .
Ameeleza kwamba kutokana na Wizara hivyo ni mpya ni vyema kukamilisha muundo wa Wizara hivyo kwa haraka ili kuweza kutekeleza majukumu yao Kwa ufanisi.
Mapema Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji wa Wizara ya Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo Rashid Hamdu Makame ameahidi kutoa mashirikiano ya pamoja Kwa Viongozi hao Kwa nia na malengo na kuleta ufanisi .

No comments