WAKULIMA WANAWAKE VIONGOZI TUMIENI VYOMBO VYA HABARI MTAKOMBOKA
Na Thuwaiba Habibu, Zanzibar
Meneja Miradi kutoka chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA-ZNZ Nairat Abdulla amewahimiza wanawake viongozi kutumia vyombo vya habari kueleza mafanikio na changamoto zinazowakabili katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya Nchi.
Ameyasema hayo wakati wa mafunzo ya wanawake viongozi juu ya kukabiliana na mabadiliko ya ya tabia ya nchi yaliofanyika katika ofisi za TAMWA Tunguu Zanzibar yenye lengo la kurejesha hali halisi ya visiwa hivyo.
Amesema wanawake viongozi wanatakiwa watumie vyombo vya habari ili waweze kuonesha mafanikio na changamoto wanazopitia katika shughuli za kimaendeleo wanazo zifanya hasa hizi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ili kupata ufumbuzi wa changamoto hizo.
Aidha aliwasihi kuwa mabalozi kwa jamii zao kuhakikisha wanakabiliana na changamoto zote za mabadiliko ya hali ya nchi ikiwemo kupanda miti,kutoharibu mazingira kwa kuchimba michanga na kuzuiya wasiharibu uoto wa asili ili kudumisha mandhari mzuri ya nchi .
Katibu wa kikundi cha Huruma hailei Mwana na Mjumbe wa sheha kutoka sheria ya bungi Salma Shija Masanja amesema kuwa baada ya kuja kwa mradi wa zan adapt katika mkoa wao wa kusini kumewasaidia wanawake wengi kujuwa mbinu mzuri za kuhifadhi mazingira kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yapo.
Nae Mkulima kiongozi kutoka Unguja ukuu kae Pwani Zakia Mansabu amesema wana mafanikio makubwa baada ya kuja kwa mradi huu wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwani wameweza kurejesha uoto wa asili na kuhifadhi mazingira kutokana elimu ya kutunza mikoko na kupatiwa miti13,887 ambayo tayari imeshapanda.
Kwa sasa tumepiga hatua katika suala zima la kukaliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwani kuna wasimamizi wa kuangalia mazingira yasihariwe na jamii inaelewa umuhimu wa jambo hili.
Pia walishukuru kupatiwa mafunzo hayo kwani yamewasaidia katika kutunza mazingira na wameahidi watahakikisha wataongeza kupanda miti na kutumia elimu hiyo kuelimisha wengine.
No comments