Breaking News

TAMWA ,YAWANOA WAKULIMA VIONGOZI KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI

Na Nafda Hindi TAMWA ZNZ

Mkuu wa mawasiliano kutoka Chama cha waandish wahabari Wanawake Tanzania, TAMWA ZNZ Safia Ngalapi amewaomba wanawake kutumia vyombo vya habari kwa lengo la kutangaza kazi zao wanazozifanya.

Akifungua mafunzo ya siku mblili yaliofanyika ofisi za TAMWA Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja, ya kuwajengea uwezo wakulima viongozi kutoka shehia nne za Unguja, katika kutumia vyombo vya habari amesema wanawake wanajishughulisha na harakati mbali mbali zikiwemo za uzalishaji pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi lakini bado sauti zao hazisikiki ipasavyo kupitia vyombo vya habari.

Hivyo amewaomba wanawake hao kutumia vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii, kuelezea mafanikio na changamoto zinazowakabili katika kupambana na mabadilikoya tabianchi ili kufikisha ujumbe kwa wahusika na hatimae kupatiwa ufumbuzi.

Mapema muwasilishaji mada inayohusu mitandao ya kijamii, kutoka TAMWA ZNZ Khairat Haji amesema mitandao ya kijamii ni njia moja wapo ya kujitangaza endapo itatumika ipasavyo hasa katika dunia hii ya sayansi na teknologia.

Aidha Khairat amesema ili kuepuka udhalilishaji kupitia mitandao ya kijamii, ni vyema kuepuka kuchapisha maisha yao binafsi kwa kulinda usalama wao na badala yake kuitumia kama njia moja ya kujiongezea kipato.

Nao wakulima viongozi  kutoka shehia nne za Unguja, Mkoa wa Kusini, ambazo ni Bungi, Unguja Ukuu, Uzi na Ng’ambwa wamesema wamefarajika kupata mafunzo hayo, na wameahidi kuwa mabalozi wazuri kwa kufikisha ujumbe kwa jamii .

Mradi  unaohusu nafasi ya mwanamke kiongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, (Zanzadapt) unatekelezwa kwa pamoja na TAMWA ZNZ, Jumuiya ya misitu Pemba (CFP), Jumuiya ya misitu Kimataifa (CFI) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Canada.


No comments