KAMATI YA ZAMECO YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUFANYIA UCHECHEMUZI SHERIA ZA HABARI
Kamati ya Wataalamu wa Maswala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) inaendelea kuwasititiza wanahabari juu ya kufanya uchechemuzi wa masuala ya sheria ya habari kwani jambo hilo bado halijapata muwafaka wake.
Hayo yamezungumzwa 8/7/2025 katika mkutano wa mapitio ya sheria ya habari uliofanyika katika ofisi za TAMWA Tunguu Zanzibar ambao uliowajumuisha wajumbe wa Kamati ya ZAMECO,Waandishi wa Habari pamoja na wajumbe wa Baraza la wawakilishi, kamati hiyo ikasema safari ya kupata sheria rafiki bado haijafika pale tunapopataka licha ya kuwa tumewasilisha jambo hili kwa njia tofauti kwa viongozi.
Aidha wamesema sheria iliyopo ni ya muda mrefu tangu 1988 na imeshapitiwa na wakati kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari ambapo inapelekea vikwazo vikubwa kwa wanahabari na kuwanyima waananchi taarifa muhimu kutokana na vikwazo vya sheria hiyo.
"Bila ya habari sio rahisi kupata maendeleo ya kweli nchi."
Nae Muwakilishi wa Jimbo la Pandani Professa Omar Fakih Hamad amesema serikali haijawahi kulikataa suala la wanahabari kupata wa sheria hiyo bali suala hilo lipo katika mikakati ya kulipatia ufumbuzi na kwa mwaka huu walitarajia itapatikana lakini halikuwezekana kutokana na bajeti.
Pia alikiri kuwa kuna haja ya kurekebishwa kwa sheria ya habari kwani toka itungwe wakati kipo chama kimoja hadi sasa teknolojia na mambo mengi yamebadilikana na inapaswa kwendana na mazingira yaliyopo.
Amesema wao kama wawakilishi wataendelea kusimamia sheria hii na wale watakao kuja watawaeleza kwani mara ya mwisho serilkali iliahidi ipo njiani na mswaada huo utawasalishwa na kupatikana kwa sheria hio.
" Awamu 5 zijazo Sheria hii ya habari itapatikana katika baraza linazolofata la 11 kwani wawakilishi watalisemezea kupitia mswaada binafsi"
Muwakilishi wa jimbo la Mfenesini Mh Machano Othmani Said amewataka waandishi kuendelea kudai sheria yao kwa amani kutokana na kiongozi aliyopo anabusara na an0afahamu umuhimu ya suala hilo na atatoa suluhisho kwa jambo hilo.
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-ZNZ aliwashukuru wawakilishi kwa kuchukua nafasi ya kulijadili mswaada wa sheria ya habari kwa lengo la kupata suluhu ya kusaidia waandishi katika hilo.
No comments