Breaking News

KUPATIKANA KWA SHERIA MPYA NA RAFIKI YA HABARI ZANZIBAR KUTALETA MAZINGIRA BORA KWA WAANDISHI NA WADAU WA HABARI NCHINI.


NA SITI ALI

Licha ya wadau mbalimbali kutoa na kuwasilisha mapendekezo yao kuhusu mapungufu yaliyopo kwenye baadhi ya sheria hizo, lakini utekelezaji wake bado umekuwa wa kusuasua jambo ambalo linapelekea mazingira magumu ya utendaji wa kazi kwa vyombo vya habari nchini.

Wadau  wa  habari nchini wamekuwa wakichukuwa jitihada mbali mbali za kuusemea na kuufatilia mchakato wa marekebisho ya mswaada wa sheria za habari uliotolewa maoni na wadau ili  kutoa mazingira rafiki kwa waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao bila vikwazo.

Mwakilishi wa wananchi jimbo la Pandani Profesa Omar Fakih Hamad amesema kuwa ni jambo la kupongezwa kwa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kulifanyia wepesi suala hili la huduma za habari ili liweze kupatikana kwa haraka kwani imekuwa ni ikisuasua jambo ambalo linashangaza wajumbe wengi wa baraza la mapinduzi.

“Mimi binafsi nimechukuwa hatua ya kulifikisha suala hili la sheria ya habari kwa Mh Spika tokea tarehe 26 Febuari 2025 nimewasilisha taarifa mbili ikiwemo hii ya kuomba kuruhusiwa kupeleka mswaada binafsi wa huduma za habari ambayo inahitaji kufanyiwa marekebisho kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa baraza la wawakilishi kanuni namba 83 na 86, na kuleta sheria mpya ambayo inaendana na wakati uliopo.Naahidi tutaendelea kusimamia pamoja na kuendeleza palipobakia ili iweze kupitishwa”alieleza Profesa Omar.

Mwakilishi wa wawananchi wa jimbo la Mfenesini Mh Machano Othman Said ameeleza kuwa ni jambo la kupongezwa kwa wadau na waandishi wa habari kuendelea kushauriana na serikali katika kwa njia ya Amani ili iweze kupitishwa kwa maslahi mapana ya wanahabari na nchi kwa ujumla .

“Nikiri kuwa zipo baadhi ya wizara ni wazito kurekebisha sheria na shauri kuendelea kudai hii sharia kwa njia ya utaratibu wa kawaida kwani waandishi wa habari ni watu muhimu katika nchi,pamoja na kuzidisha mashirikiano baina yenu na kuahidi kuipitisha katika awamu ijayo ili kutumika kwa maslahi ya taifa”ameeleza Mh Machano.

Vile vile Mwakilishi wa wananchi jimbo la Mtambwe Daktari Muhammed Ali Suleiman amesema kuwa wataendelea kuipambania na kuishauri serikali kuifanyia marekebisho sharia hii ya habari ili iweze kufanikiwa kwa maslahi ya waandishi wa habari na serikali kwa ujumla.

 “Tutaendelea kuipambania na kuishauri serikali kuifanyia haraka marekebisho sheria hii ya habari ili iweze kupitishwa na kufanikiwa kwa maslahi ya waandishi wa habari na serikali kwa ujumla”alieleza Dr Muhammed.

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), Dkt. Mzuri Issa amefarijika kwa kuona wawakilishi wa vyama mbali mbali vya siasa na wadau wa habari kuwa vinaunga mkono juhudi zinazotolewa na wadau wa habari katika kuisemea pamoja na kutoa motisha ili kuupitishwa mswaada wa sharia ya habari Zanzibar japo kuwa haijafanikiwa lakini ipo katika hatua nzuri.

“Nimefarijika kwa kuona wawakilishi wa vyama mbali mbali vya siasa na wadau wa habari kuwa vinaunga mkono juhudi zinazotolewa na wadau wa habari katika kuisemea pamoja na kutoa motisha ili kuupitishwa mswaada wa sheria ya habari Zanzibar japo kuwa hatujafanikisha lakini ipo katika hatua nzuri”anaeleza Dr Mzuri.

Sambamba na hayo Dr Mzuri ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Hussein Ali Hassan Mwinyi kwa kuwapa kipao mbele katika masuala ya sharia kwani hii inatokana na waandishi kupata shida katika kipindi cha uchaguzi .

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa ZAMECO mjumbe katika kamati hiyo Bishifaa Said Hassan ameelezea mashirikiano yaliopo baina yao na wawakilishi pamoja na kuahidi kuzidisha umoja na mashirikiano yao ili kuweza kufanikisha azma yao ya kuupitisha mswaada wa sheria mpya ya habari ili iweze kupatikana kwa maslahi ya nchi na taifa kwa ujumla.

“Kwa upande wetu mashirikiano yamezidi baina yetu na wawakilishi ili kuweza kufanikisha azma yetu ya kuupitisha mswaada wa sheria mpya ya habari ili iweze kupatikana kwa maslahi ya nchi na taifa kwa ujumla”anaeleza Bishifaa.

Licha ya hatua nzuri iliyofikiwa lakini ni vyema kwa waandishi wa habari kuzidisha mashirikiano baina yao kwa kuendelea kufuatilia Zaidi pamoja na kukumbushana hususani katika kipindi hichi cha kuelekea kwenye uchaguzi.



No comments