MATUMAINI YA UPATIKANAJI WA SHERIA MPYA ZA HABARI ZANZIBAR UMELETA SURA KWA WAANDISHI WA HABARI NA TASNIA YA HABARI KWA UJUMLA.
NA SITI ALI.
Takribani ni miaka kadhaa waandishi wa habari Zanzibar wamekuwa wakilalamikia upatikanaji wa sheria mpya za habari hali ambayo inawapa wasiwasi na hofu katika kazi zao
Wadau mbali mbali wa vyombo vya habari wamekuwa wakifuatilia mchakato wa marekebisho ya sheria za habari zilizotolewa maoni ili kutoa mazingira rafiki kwa waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao bila vikwazo.
Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA ZANZIBAR)wamekuwa wakichukuwa jitihada mbali mbali za kutoa uchechemuzi wa masuala ya sheria za habari ikiwemo kuandaa mafunzo kwa waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Unguja na Pemba ili kuongeza ufanisi katika kazi zao.
Afisa mradi wa msuala ya sheria kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA ZNZ)ndugu Zaina Abdallah Mzee ameelezea mafanikio waliyoyapata kwenye upatikanaji wa sheria ya habari na uhuru wa kujieleza ikiwemo kuwajengea uwezo waandishi wa habari kwa kutoa elimu kwa wanajamii na kueleza changamoto zilizomo kwenye sheria za habari pamoja na kupaza sauti zao kwa kuwaelimisha wanajamii kuhusu uhuru wa kujieleza kwa lengo la kuleta mabadiliko katika tasnia ya habari.
“Mafanikio ni mengi tuliyoyapata kwenye upatikanaji wa sheria ya ya habari na uhuru wa kujieleza ikiwemo kuwajengea uwezo waandishi wa habari kwa kutoa elimu kwa wanajamii na kueleza changamoto zilizomo kwenye sheria za habari pamoja na kupaza sauti zao kwa kuwaelimisha wanajamii kuhusu uhuru wa kujieleza kwa lengo la kuleta mabadiliko katika tasnia ya habari ”ameelezea Zaina.
Pia Afisa huyo amesema kuwa wajumbe wa kamati ya wataalamu wa masuala ya habari Zanzibar (ZAMECO)wamefanya mambo makubwa ya uchechemuzi na kuwashawishi baadhi ya viongozi wa serikali na wajumbe wa baraza la wawakilishi kuweza kupatikana kwa sheria mpya ya habari japo haikupatikana lakini kuna mabadiliko makubwa kwa lengo la upatikanaji wa sheria mpya ya habari.
“Wajumbe wa kamati ya wataalamu wa masuala ya habari Zanzibar (ZAMECO)wamefanya mambo mengi ya uchechemuzi na kuwashawishi baadhi ya viongozi wa serikali na wajumbe wa baraza la wawakilishi kuweza kupatikana kwa sheria mpya ya habari japo haikupatikana lakini kuna mabadiliko makubwa kwani zipo ahadi nyingi zilizowekwa za upatikanaji wa sheria mpya ya habari”amesema Afisa huyo.
Hata hivyo Zaina amesema mbali ya mafanikio hayo yaliyopatikana lakini pia zipo changamoto zinazopatikana kwa waandishi wa habari ikiwemo kutopatikana kwa sheria mpya ya habari hususani katika kipindi hichi cha kueleke kwenye uchaguzi kutokana na usalama wa waandishi wa habari,pamoja na kutoa wito kwa viongozi wataoingia madarakani kulifanyia wepesi suala hili la sheria mpya ya habari liweze kukamilika ili kuwasaidia waandishi kufanya kazi zao bila ya woga.
Kaimu mwenyekiti wa uchechemuzi wa TAMWA ZANZIBAR Bishifaa Said Hassan amesema kuwa wamefanya mambo mbali mbali ya uchechemuzi kwa waandishi wa habari kujua sheria zao kuandika na kutoa vipindi mbali mbali na kuwashawishi baadhi ya viongozi wa serikali na wajumbe wa baraza la wawakilishi na kusema kuwa muamko ni mkubwa kwa waandishi wa habari kuzitumia kalamu zao kwani hatua iliyofikiwa ni nzuri na kuwataka kushirikiana kwa pamoja ili kulifanikisha jambo hilo.
“ Mafanikio ni mengi tuliyoyapata waandishi wa habari ikiwemo kujua sheria kwa kutumia kalamu kuandika na kutoa vipindi mbali mbali vinavyohusu sheria ya habari na kuwashawishi baadhi ya viongozi wa serikali na wajumbe wa baraza la wawakilishi na wadau wa habari na kusema kuwa muamko ni mkubwa kwani hatua iliyofikiwa ni nzuri tushirikiane kwa pamoja ili kulifanikisha jambo hilo”amesema Bishifaa.
Mjumbe wa kamati ya wataalamu wa masuala ya habari Zanzibar (ZAMECO)ndugu Abdallah Mfaume amesema kuwa wana matumaini makubwa na awamu ijayo kuipata sheria hii mapema ili kuwafanya waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi ,sambamba na kutoa wito kwa waandishi wa habari kufuata kanuni na sheria pamoja na misingi iliyowekwa ili kufanya kazi kwa usalama.
“Tunamatumaini makubwa na awamu ijayo kuipata sheria hii mapema kabla ya kumalizika kuipata sheria mpya ya habari ambapo itawafanya waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi ,wito wangu kwa waandishi wa habari kufuata kanuni na sheria pamoja na misingi iliyowekwa ili kufanya kazi kwa usalama”amesema Abdallah Mfaume.
Mradi wa sheria ni mradi wa majaribio wa miaka miwili unaotekelezwa na chama cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na wadau wa habari ,na waandishi wa kujitegemea mbapo umefadhiliwa na Comman Wealth una lengo la kupata sheria mpya ya habari, uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza ukuwe na kuheshimika, jumla ya waandishi 25 wa Unguja na Pemba walipatiwa mafunzo na kufanikiwa kuandika stori na Makala 253 katika vyombo mbali mbali ilkiwemo TV,redio,magazeti na mitandao ya kijamii .


No comments