Breaking News

HUU NDIO UMUHIMU WA USHIRIKI WA BABA KATIKA UZAZI WA MPANGO

 


NA SITI ALI.

KATIKA wanaume wanne kati ya watano duniani wanaweza kuwa baba kwa namna moja ama nyengine katika maisha yao .lakini suala la kupata mtoto linawahusu watu wawili yaani mwanamke na mwanamme.

Uzazi wa mpango ni maamuzi ya hiari ambayo yanawahusu baba na mama ambao huamua watoto wao wapishane kwa muda gani na inasisitizwa angalau iwe kwa miaka miwili kama tulivyoamrishwa katika dini na Mtume Muhammad (S.A.W).Hata hivyo wanaume wengi hawashiriki katika suala zima la uzazi wa mpango kutokana na sababu mbali mbali.

Daktari Zuhura Saleh Amour ni Msaidizi meneja katika kitengo cha maradhi yasiyoambukiza kutoka hospitali ya Mnazi Mmoja ameelezea faida mbali mbali zinazopatikana katika familia pindi tu wanaume wanaposhiriki katika uzazi wa mpango ikiwemo kuongeza upendo katika familia,kuwa na watoto wenye afya njema,kuwakinga watoto na maradhi ikiwemo utapia mlo,kuepusha migogoro isiyo ya lazima kama vile kushindwa kuwahudumia pamoja na kupata maendeleo katika familia.

Faida nyengine ni kuongeza kipato na uchumi katika familia,baba kupata nafasi ya kuwa mlezi mzuri katika familia,kutokuwa na dhana potofu,kumpa uhuru mama kuchagua njia inayomfaa kutumia.

“Faida zinazopatikana katika familia pindi tu wanaume wanaposhiriki katika uzazi wa mpango ni pamoja na kuongeza upendo katika familia,kuwa na watoto wenye afya njema,kuwakinga watoto na maradhi ikiwemo utapia mlo,kuepusha migogoro isiyo ya lazima kama vile kushindwa kuwahudumia pamoja na kupata maendeleo katika familia.

Faida nyengine ni kuongeza kipato na uchumi katika familia,baba kupata nafasi ya kuwa mlezi mzuri katika familia,kutokuwa na dhana potofu,kumpa uhuru mama kuchagua njia inayomfaa kutumia”anaeleza Daktari Zuhura.

Kuna hatua mbali mbali za kuchukuwa pindi baba atakaposhiriki uzazi wa mpango kama vile kupata elimu ya afya kwa usahihi inayohusu uzazi wa mpango,kuwa tayari kupata maelekezo ya wataalamu wa afya ya uzazi wa mpango,kuwa balozi kwa wanaume wenzake juu ya utumiaji uzazi wa mpango,kuhudhuria klinikkwa pamoja kupata ushauri wa njia sahihi za uzazi wa mpango,kuzidisha upendo kwa mwenza wake kwa hali na mali.

Licha ya serikali na wizara kutoa elimu kwa wanajamii juu ya matumizi ya uzazi wa mpango lakini bado kuna changamoto za wanaume wasioshiriki katika uzazi wa mpango jambo ambalo linarudisha nyuma ustawi wa jamii kama vile kuendekeza mila na desturi,kutokuwa na elimu ya uzazi wa mpango Imani potofu zinazotokana na njia za uzazi wa mpango mfumo dume na mengineyo.

Hata hivyo hasara mbali mbali hupatikana pindi baba asiposhiriki uzazi wa mpangoikiwemo ongezeko la vifo vya mama na mtoto,utoaji wa njia zisizo salama,kupelekea msongo wa mawazo,mama na mtoto kutokuwa na afya bora migogoro isiyo ya lazima katika familia, kubeba mimba bila ya kutarajia,kukosekana kwa uaminifu katika ndoa,kupelekea ukatili wa kijinsia kwa mwanamke.

Waziri wa afya Zanzibar Muheshimiwa Nassour Ahmed Mazrui katika uzinduzi wa kampeni ya malezi makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto Zanzibar amesema kuwa ni jukumu la kila mtu kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika malezi na makuzi ya mtoto ili kupata taifa bora lenye misingi ya Amani na utulivu.

“Kila mtu ana haki ya kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika makuzi ya mtoto tokea atakavyokuwa tumboni hadi anapozaliwa wakiwa na afya bora tabia njema na uadilifu hivyo ni vyema kushirikiana kwa pamoja kulea watoto ambao watapelekea kuwa na siha na tabia njema kwani malezi bora ni msingi wa Amani”amesema Waziri Mazrui.

Bwana Khamis Juma Mwalimu mkaazi wa Mfenesini ni mwanamme ambaye anatumia uzazi wa mpango ameelezea faida wanazozipata mara tu baada ya kutumia uzazi wa mpango ikiwemo kuongeza kipato na uchumi katika familia, kuwa mlezi mzuri katika familia,kutokuwa na dhana potofu,kumpa uhuru mama kuchagua njia inayomfaa kutumia,pamoja na kutoa wito kwa wanaume wenzake kutumia uzazi wa mpango ili kuleta ustawi katika jamii.

“Mimi na mke wangu tumepata faida nyingi tulipoanza kutumia uzazi wa mpango wanazozipata mara tu baada ya kutumia uzazi wa mpango ikiwemo kuongeza kipato na uchumi katika familia, kuwa mlezi mzuri katika familia,kutokuwa na dhana potofu,kumpa uhuru mke kuchagua njia inayomfaa kutumia,natoa wito kwa wanaume wenzangu kushiriki katika kutumia uzazi wa mpango ili kuleta ustawi katika jamii”anaeleza Bwana Khamis.

 Bi Aisha Ali Salim mkaazi wa Mfenesini ni mke wa Bwana Khamis Juma ambao wanatumia uzazi wa mpango anaelezea jinsi alivyofarijika baada ya kuanza kutumia uzazi wa mpango ambao umewasaidia kuongeza kipato katika familia yao.

“Nimefarijika sana baada ya mume wangu kukubali kushiriki katika uzazi wa mpango kwani ni jambo la furaha na faraja kwetu na familia kwa ujumla”amesema Bi Aisha.

Wizara ya afya Zanzibar pamoja na vitengo vyake vimekuwa vikichukuwa jitihada mbali mbali za kuweka afya bora kwa mama na mtoto kwa kutoa elimu juu ya suala zima la ushiriki na ushirikishwaji wa baba katika uzazi wa mpango jambo ambalo ni linaleta mafanikio katika nchi na taifa kwa ujumla.

Ewe baba shiriki kikamilifu katika uzazi wa mpango ili kupata taifa bora lenye wasomi pia kuipunguzia serikali mzigo wa gharama za matibabu kwa wananchi kwani uzazi wa mpango ni jukumu la kila mtu.



No comments