Breaking News

“HATUJAPATA BOTI ZA UCHUMI WA BULUU”

  


Said Khamis. 27/11/2025.  

‎Wavuvi wa shehia ya Nungwi wameiomba serikali kupitia wizara ya uchumi wa buluu kuwapati vifaa vya kisasa vya uvuvi ili kuweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.

‎Wakizungumza na TOZ baadhi ya wavuvi walisema licha ya serikali kutoa boti za kisasa za uvuvi pamoja na vifaa lakini kwa upande wao hawajapata vifaa hivyo wala boti.

‎Walieeleza kuwa lengo lao kubwa nikuona nawao wanapatiwa boti hizo kama walipewa wavuvi wengine ili kuweza kuvua katika bahari Kuu.

‎" Wavuvi wenzetu wamenufaika na boti walizopewa na sisi serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Mhe.Dk Hussein Ali Mwinyi awamu hii tupatiwe wavuvi wa nungwi wapo baadhi ya wavuvi wenzetu ila hatufaham wamepata kwa njia gani " walisema wavuvi



‎Sambamba na hayo waliongeza kusema kwamba wanaomba kupatiwa boti nyengne za uwokozi ili panapotokea majanga waweze kufika kwa haraka eneo la tukio.

‎Katibu wa Uvuvi wa shehia hiyo Bw. Khamis Hafidh Ali aliongeza kusema kuwa licha ya idara ya uvuvi kuwapatiwa mafunzo wavuvi kuweza kuepukana na uvuvi haramu lakini bado kwa upande wao hawajanufaika na boti zakisasa zinazotolewa na uchumi wa buluu.

‎" Tunaishukuru idara kutupatia mafunzo endelevu yakuweza kuvua samaki kwa njia zinazotakiwa lakini ninaomba wavuvi wetu tuwapate boti za kisasa kwani bado wanaendelea kuvua kizamani " Alisema Katibu.



‎Aidha Khamis ameiomba serikali kuwapunguzia masharti magumu pindi wanapopatiwa boti hizo kwani asimilia kubwa ya wakaazi wa nungwi wanategemea shughuli za uvuvi katika maisha yao ya kila siku.


No comments