Breaking News

Ziara za Dkt. Mwinyi Qatar, Hispania na Armenia Kufungua Fursa Mpya za Maendeleo Zanzibar


NA SITI ALI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema ziara zake nchini Qatar, Hispania na Armenia zimefungua fursa mpya za uwekezaji, maendeleo ya michezo na uhifadhi wa mazingira kwa Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 18, 2026, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume baada ya kurejea nchini, Rais Mwinyi amesema kampuni ya Alfardan kutoka Qatar imeonesha nia ya kuwekeza Zanzibar katika sekta ya hoteli, makaazi na miradi mingine ya maendeleo. 

Katika ziara ya Hispania, amesema makubaliano kati ya Real Madrid Foundation na Unicorn Zanzibar Sports Limited yanalenga kukuza vipaji vya soka kwa vijana, kutoa mafunzo kwa makocha na kuweka msingi wa kuanzishwa kwa Real Madrid Academy Zanzibar.


Aidha, akiwa Armenia, Rais Mwinyi amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto za mazingira, ikiwemo mmomonyoko wa fukwe, upungufu wa maji na kulinda rasilimali za bahari.

Amesema mafanikio ya ziara hizo yatategemea utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa ili kuleta matokeo halisi katika uwekezaji, ajira, michezo na uhifadhi wa mazingira kwa maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

 

 


1 comment: