Breaking News

WAFANYA BIASHARA WATAKIWA KUFANYA BIASHARA MAENEO RASMIN.









































Na Said Khamis                                                                                                                Wafanyabiashara wametakiwa kufanya Biashara zao maeneo rasmin badala ya  kueka Biashara pembezeni mwa barabara kwa ajili ya usalama wao na mali zao.
‎Wito huo aliutoa Msatahiki Meya wa Baraza la Manispaa Kati Said Hassan Shaaban katika muendelezo wa mikutano na Wafanyabiashara wa Wilaya hiyo hafla iliyofanyika katika        Ukumbi wa Baraza la Manispaa Kati Dunga.                                                                                         
‎Alisema wafanyabiashara wanatakiwa kuyatumia masoko yaliyojengwa na serikali ili kuweza kufanya Biashara hizo katika mazingira mazuri na salama kwa kufanya shughuli hizo.
Meya huyo alimesema kwamba tayari wafanyabiashara hao wamekuballiana  kufanya 'biashara sehemu rasmini kwa maslahi yao na kwaajili ya kuingizia serikali mapato.                    
‎Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Mapato Uchumi na Wajasiriamali Baraza la Manispaa Kati Mussa Abdurab Fadhil alisema miongoni mwashughuli kubwa ya baraza hilo ni kuwasimamia wafanyabiashara katika suala zima la usafi katika sehemu zao za biashara hivyo wameona kila sababu wanyabiashara kufanya shughuli hizo sehemu rasmin.                          
Mussa aliendelea kusema kuwa  baadhi ya Wafanyabiashara hufanya shughuli hizo sehemu hatarishi ikwemo pembeni mwabarabara ambapo wanahatarisha usalama wao na mali zao .
''Unakuta mfanyabiashara anaeka biashara pembeni mwabarabara gari inaweza kuacha njia au chombo chochote cha moto kikamsababishia hasara yeye mwenyewe bianfsi au kuharibu

mali yake'' alisema Mussa
‎Nao baadhi ya Wafanyabiashara wa dunga mitini walieleza kuwa sababu inayowanya kutolitumia soko la wajasiriamali Dunga ni kutokana na kuwepo mzunguko mdogo wa wateja wanaokwenda katika soko hilo.                                                                                                           
''Dunga mitini panamzunguko wa biashara kwani gari zote za zinazokwenda kusini na kaskazini zinapita hapo lakini Dunga skuli hakuna biashara kutokana hakuna mzunguko mkubwa wa watu wala kiyuo rasmin cha kushusha na kupakia abiria'' Walisema wafabiashara
‎Zaidi ya Wafanyabiashara 15 pamoja na watendaji wa baraza hilo wamehudhuria katika Mkutano huo wenye lengo la kuwaekea mazingira rafiki wafanyabiashara ili kuweza kujiongezea kipato na kujikwamua na hali ngumu ya kiuchumi.


No comments