Breaking News

ZAECA YATOA MUDA WA WIKI MBILI KUREJESHWA FEDHA ZA FIDIA ZILIZODAIWA KUPOTEA.



Na Siti Ali.
Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA) imetoa muda wa wiki mbili kwa mwananchi yeyote anayehusika katika ubadhirifu wa fedha au mali zinazohusiana na malipo ya fidia ya Serikali, kuhakikisha anarejesha fedha au mali hizo ndani ya kipindi hicho.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 14, 2026 na Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA, Ali Abdalla Ali, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za mamlaka hiyo zilizopo Kilimani, Zanzibar.

Amesema hatua hiyo imefuatia ripoti iliyowasilishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambapo baada ya kupitia ripoti hiyo, alitoa maelekezo ya kurejeshwa kwa fedha zilizopotea pamoja na kuitaka ZAECA kusimamia utekelezaji wa suala hilo kwa mujibu wa yaliyoainishwa katika ripoti hiyo.

Aidha, ZAECA imeeleza kuwa muda huo wa wiki mbili utaanza leo Mei 14, 2026 na kumalizika Mei 28, 2026, huku ikiwasisitiza wote waliohusika kutumia fursa hiyo kurejesha fedha au mali husika kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa

No comments