Breaking News

TUNATAKA DIRA ITAKAYOKOMBOA MWANATAALUMA NA KUIMARISHA UTAWALA BORA ''OMO''



Na Siti Ali

Makamu wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar,  Othman Masoud Othman ameutaka Uongozi wa Kamati ya Kuandaa Dira ya Maendeleo ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar University  (Zanzibar Univwersity) (ZU) kutathmini kwa kina matatizo yanayoikabili Jamii, ndani ya mazingira ya masomo na nje ya mazingira hayo ili kuimarika na kueka sawa maeneo yote ya kitaaluma.
 
Akizungumza na Ujumbe huo uliofika Nyumbani kwake  Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar,  katika Muendelezo wa kukutana na viongozi wakuu wa Nchi na Watu Mashuhuri, ambapo ni muendelezo wa zoezi  la kukusanya maoni kwa ajili ya uundwaji wa  Dira ya Maendeleo ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha 'Zanzibar.

Amesema iwapo sera na utawala bora vitakuwepo nchini,  mwalimu atalipwa vizuri, wanafunzi watapata elimu bora na miundombinu rafiki na huduma nyengine zitaimarika.  
 ''Hakutokuwa na migogoro wala mianya ya kuwatumia wanafunzi nje na matumizi ya kielimu", amefahamisha. 



Amefahamisha wajibu wa Serikali  wa kuhakikisha mazingira ya kielimu yanakuwa rafiki kutoka ngazi za juu hadi kuwafikia wanafunzi wa chini. 

Mwenyekiti wa kamati hiyo Omar Juma Mustafa,  amesema maoni wanayo endelea kuyakusanya, watayafanyia kazi kwaajili ya kusaidia maendeleo, na  kujenga mustakbali mwema wa aanachuo, kutengeneza Serikali ya Wanafunzi iliyo bora na hasa katika Uundaji wa dira hiyo yenye Lengo la kumkomboa kila Mwanataaluma.
dira hiyo itakuwa ni chachu ya maendeleo kwa wanafunzi, wakiwa masomoni hata baada ya kitimu masomo yao.



No comments