Breaking News

NGUVU YA ZIADA YAHITAJIKA KUELIMISHA WANAWAKE KUPIMA SARATANI



Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa wilaya ya kati Rajab Ali Rajab amesema bado  juhudi za makusudi zinahitajika. Kuielemisha jamii juu ya umuhimu wa kufanya uchunguzi wa mara Kwa mara Kwa magonjwa ya saratani hasa ya shingo ya kizazi na matiti Ili kupunguza kasi ya ongezeko la ugonjwa huo

Ametoa kauli hiyo huko Dunga ukumbi wa uhamiaji  katika mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo katika ngazi za jamii na wahudumu wa afya ngazi za msingi yaliyoandaliwa na taasisi ya JAPAIL ya Daresalam ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa mradi wa taasisi hiyo.

Amesema  ugonjwa huo badoni tatizo Kwa  jamii Kwa vile bado jam Haina uwelewa na mwamko wa kotosha  juu ya kufanya uchunguzi wa  mapema  hali inayipelekea ugonwa huo kuongezeka Kwa Kasi kutokana  watu wengi wanapokwenda  hospitali kufanya uchunguzi  hua tayari wameshachelewa.

Aidha  amesema serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa  katika  sekta ya afya Kwa  kuimarisha  miundombinu na vifaa   tiba hivyo    ameiataka jammi kufuata huduma za masuala  mbali mbali ikiwemo uchunguzi wa afya zao Ili kujibaini na mapema huku akiwataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia mafunzo wanayopatiwa na na kuyaeneza Kwa jamii Ili  iweze kuondokana na athari za magonjwa mabli mbali ikiwemo iyo ya saratani.

Daktar wa uchunguzi  kutoka hospital ya wilaya Mwera pongwe ndugu said Abdallah Ali amesema ugonjwa wa saratani unatibika iwapo utagundulikana na mapema lakini kumekuwa na tabia Kwa baadhi ya watu kwenda hospitali tatizo limeshakua kubwa na kushindwa kutibika, hivyo ameitoa hofu jamii na kuishauri kufika hospitali na mapema pindi wanpojigundua  Wana dalili za ugonjwa huo Ili kupatiwa matibabu Kwa wakati.

Nae afisa wa mradi wa JAPAIL BI Harrieth khamis ameisifu juhudi zinazoendelea kuchukuluwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar ya kutoa huduma na  matibabu Bure zinazohusiana na ugonjwa wa saratani  na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo Ili kuona ugonjwa wa saratani ya matiti unapungua Kwa wananchi wa zanzibar na Tanzania Kwa ujumla.

Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema utolewaji wa mafunzo hayo utasaidia jamii kupata uwelewa juu ya hatari ya kutokufanya uchunguzi na  mapema na kuahidi kueneza elimu hiyo Kwa jammi Ili kuona  lengo lililokuaudiwa linafikiwa.

Mafunzo hayo ya siku moja yamewaahirikisha viongozi wa masheha,madiwani,wahudumu wa Afya na viongozi dini yana lengo la kuielemisha jamii juu ya umuhimu wa kufanya uchunguzi na mapema juu ya ugonjwa wa saratani  ya matiti na shingo ya kizazi.

JE WEWE UMEPIMA? Tuandikie kwenye comment.



No comments