Breaking News

KAENI VIKUNDI KUPATA MIKOPO YENYE TIJA. DK MWANAISHA.

 

Na Said Khamis.
Wafanyabiashara pamoja wajasiriamali wa wilaya ya kati wametakiwa kujikusanya pamoja ili kuweza kupatiwa mikopo yenye masharti nafuu kwalengo la kujikwamua kiuchumi.

‎Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Kati Dk Mwanaisha Ali Said katika mkutano wa wafanyabiashara wa soko la Dunga uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa Kati Dunga.

‎Amesema mkutano huo umelenga kujadili changamoto zilizopo katika soko hilo na kuweza kuzipatia ufumbuzi hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kujisajili ili kuweza kupatiwa mkopo hiyo yenye masharti nafuu.

‎Dk Mwanaisha amewataka wafanyabiashara hao kuimarisha usafi wa soko, kulipa ada kwa wakati pamoja na kuhakikisha biashara zao wanaeka sehemu rasmin  walizopangaiwa ili soko hilo liwe kwenye haiba nzuri,
 

‎Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Baraza la Manispaa Kati Said Hassan Shaaban amesema changamoto kubwa iliyokuwepo kwa muda mrefu nikutoelewana kati ya manispaa na wafanyabiashara hususani katika kufuata taratibu na miongozo iliyowekwa na baraza hilo ambazo kwa sasa tayari wameshazipatia ufumbuzi.

‎Akizungumza kwaniaba ya wafanyabiashara wenzake Yussuf Issa Ali wameahidi kuyafanyia kazi maagizo na masharti waliyopewa katika kulitumia vizuri soko hilo ikiwemo kuimarisha usafi na kueka biashara zao maeneo rasmin waliyopangiwa.






‎Mkutano huo umewashirikisha viongozi wa Baraza la Manispaa kati, wafanyabiashara lengo nikujadili changamoto za soko na namna yakuweza kuzitatua changamoto hizo.

5 comments: