Breaking News

SIKU YA REDIO DUNI, NINI KIFANYIKE KUPATA HABARI ZA UCHAMBUZI?


Na Safia Makame.

 Leo tarehe 13 Februari 2026, Zanzibar imeungana na dunia kuadhimisha Siku ya Redio Duniani, siku iliyotangazwa na UNESCO mwaka 2011 na kupitishwa rasmi na Umoja wa Mataifa mwaka 2013.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Redio na Uaminifu” (Radio and Trust) – ikisisitiza kuwa uaminifu ndio msingi wa taaluma ya habari. Redio haitegemei tu nguvu ya mawimbi yake, bali imani na uaminifu wa wasikilizaji wake.

Kwa mujibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, zaidi ya vituo 30 vya redio vinafanya kazi Zanzibar. Hata hivyo, mafanikio ya sekta ya redio hayapimwi kwa idadi ya vituo pekee, bali kwa ubora wa maudhui, uhuru wa uhariri na uwezo wa kuwa sauti ya wananchi – hasa wale wa maeneo ya vijijini.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova, aliwahi kusema kuwa redio ndicho chombo cha habari kinachowafikia watu wengi zaidi duniani na ni cha gharama nafuu.

Naye aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, alisisitiza kuwa hakuna anayepaswa kubeza umuhimu wa vyombo vya habari huru katika demokrasia.

Wadau wa habari Zanzibar wametoa wito wa kuimarishwa kwa sheria za habari, kulindwa kwa waandishi wa habari, na kuanzishwa kwa chombo huru cha usimamizi wa vyombo vya habari ili kuimarisha demokrasia na haki ya wananchi kupata taarifa.

Kama alivyosema mwanahabari mashuhuri Walter Cronkite:
“Uhuru wa vyombo vya habari si jambo muhimu tu kwa demokrasia – ndio demokrasia yenyewe.”


No comments