MIAKA 62 YA MAPINDUZI ZANZIBAR YAIPAISHA SEKTA YA ELIMU
NA SITI ALI.
Mapinduzi ya Januari ya mwaka1964 ni tukio muhimu katika
historia ya Zanzibar ambapo ni mwanzo wa safari ya maendeleo ya kisiasa,
kiuchumi na kijamii. Kwa maana hiyo, maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ni
kutathmini mafanikio na malengo ya Mapinduzi kwa dhamira ya waasisi ambayo ni
kujikomboa na kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
Mwaka huu wa 2026, nchi ya inatimiza miaka 62 ya Mapinduzi ikiwa
na kauli mbiu isemayo: Amani na Umoja, Ndio Msingi wa Maendeleo Yetu,
“Mapinduzi Daima”. Kauli mbiu hii inayakisi mafanikio makubwa ambayo yamepatikana
katika nchi tokea Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964, yametokana na msingi wa
amani na umoja na jitihada za viongozi wa Awamu zote za uongozi hapa Zanzibar
na ushirikiano mkubwa wa wananchi.
Serikali ya Awamu ya Nane ilipoingia madarakani mwaka 2020,
iliahidi kudumisha mafanikio ya Awamu zilizotangulia za uongozi na kuyatafsiri
malengo ya Mapinduzi kwa vitendo kwa kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi,
kisiasa na kijamii na kuimarisha misingi ya amani, umoja na mshikamano kwa
manufaa ya wananchi wote.
Maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ikiwa ni mwanzo wa
kipindi cha pili cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nane. Ambapo imeelezea
vipaumbele na mwelekeo wa mipango ya Serikali kwa kipindi cha pili.Ambapo kwa
muhtasari mafanikio na mwelekeo wa mipango ya Serikali kwa kipindi cha mwaka
mmoja ujao.
Akilihutubia Taifa katika Maadhimisho ya miaka 62 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mheshimiwa Daktari Hussein Ali Hassan Mwinyi amesema kuwa serikali ya
awamu ya nane imejipanga kuimarisha huduma kwa jamii ikiwemo elimu,ambayo ni
miongoni mwa malengo ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Serikali imeifanya
sekta ya elimu kuwa kipaumbele kwa kuzingatia umuhimu wake katika kuandaa nguvu
kazi na kuchochea maendeleo ya nchi.
“Mageuzi makubwa yaliyofanywa na Serikali katika sekta ya
elimu ya ujenzi wa Skuli za kisasa zikiwemo za ghorofa 35, upatikanaji wa vifaa
vya kujifunzia, na kufundishia, vifaa vya maabara za masomo ya sayansi na
teknolojia, ajira mpya za walimu na kuwapatia mafunzo, kumechangia kwa kiasi
kikubwa kuimarisha mazingira ya Skuli na kuongeza kiwango cha ufaulu wa
wanafunzi katika mitihani ya Taifa.
Kwa lengo la kuendelea kuimarisha sekta ya elimu, Serikali
itaendeleza ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa kujenga Skuli za kisasa za
ghorofa ili kukabiliana na changamoto ya msongamano wa wanafunzi madarasani”ameeleza
Mheshimiwa Raisi Daktari Mwinyi.
Aidha amesema kuwa Katika kwenda sambamba na mageuzi ya
elimu wa mtaala mpya, jumla ya Skuli 70 zitaunganishwa na mkonga wa
mawasiliano, kompyuta 2,000 za mezani zitatolewa kwa ajili ya maabara za Skuli,
laptop 4,000 zitatolewa kwa ajili ya wanafunzi na kuanzisha smart classrooms 25
ili kuimarisha kujifunza na kufundisha kwa kutumia TEHAMA.
Pamoja na kusema kwamba Kwa mwaka 2025/2026, Serikali
imepanga kuajiri walimu wapya 1,500 ili kupunguza tatizo la uhaba wa walimu
hasa wa masomo ya sayansi. Aidha, tutaendeleza ujenzi wa dakhalia za wanafunzi
na utoaji wa mafunzo ya walimu ili kuwaongezea maarifa pamoja na kuimarisha
maslahi yao.
Vile vile, tunaongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu ili
kuwezesha wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu kutapa huduma hiyo kwa uhakika
“Jumla ya Skuli 70 zitaunganishwa na mkonga wa mawasiliano,
kompyuta 2,000 za mezani zitatolewa kwa ajili ya maabara za Skuli, laptop 4,000
zitatolewa kwa ajili ya wanafunzi na kuanzisha smart classrooms 25 ili kuimarisha
kujifunza na kufundisha kwa kutumia TEHAMA.
Kwa mwaka 2025/2026, Serikali imepanga kuajiri walimu wapya
1,500 ili kupunguza tatizo la uhaba wa walimu hasa wa masomo ya sayansi. Aidha,
tutaendeleza ujenzi wa dakhalia za wanafunzi na utoaji wa mafunzo ya walimu ili
kuwaongezea maarifa pamoja na kuimarisha maslahi yao.
Tunaongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu ili kuwezesha
wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu kutapa huduma hiyo kwa uhakika”amesema
Daktari Mwinyi.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika kikao cha tathmini miaka 62 ya mapinduzi ya Zanzibar
huko katika ukumbi waSheikh Idrisa Abduli wakili Kikwajuni Makamo wa Pili wa Raisi
wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amefafanuwa kuwa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar imefanikiwa kufunguwa miradi 64, ambapo iliyowekwa mawe ya msingi ni
46 kwa Unguja na 68 Pemba miradi 42 hivyo hatuwa hizo zinakuja kwa makusudi
kuboresha maeneo yete sekta ya elimu
“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanikiwa kufunguwa miradi
mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, miradi 64, imefunguliwa ambapo
iliyowekwa mawe ya msingi ni 46 kwa Unguja na 68 Pemba miradi 42 hivyo hatuwa
hizo zinakuja kwa makusudi kuboresha maeneo yete sekta ya elimu ambapo ni
maendeleo makubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma”amesema Mheshimiwa Hemed.
Bwana Khamis Juma Kombo mkaazi wa Vikokotoni ameelezea
mapinduzi ya mwaka 1964 kupitia sekta ya elimu ambapo imeleta mabadiliko
makubwa na amesema kuwa kabla ya
mapinduzi kwa upande wao ilikuwa suala la elimu ni ndoto walioishi nao na
haikuwa rahisi kuitimiza kwa kuwa ilikuwa ni ya watu maalumu ingwawa walikuwa
na hamu ya kutimiza malengo yao kupitia sekta hiyo
Hivyo walilazimika kufanya kazi zilizokuwa za nguvu kwani elimu
wakipata watu wenye hadhi na muonekano maalumu ambao ni wenye uwezo wa kifedha
na kiutawala hukuwao wakifanya kazi za kitwana ikiwemo ulinzi na ukulima.
“Kabla ya mapinduzi kwa upande wetu ilikuwa suala la elimu
ni ndoto tulioishi na haikuwa rahisi kuitimiza kwa kuwa ilikuwa ni ya watu
maalumu ingwawa tulikuwa na hamu ya kutimiza malengo yetu kupitia sekta hiyo
Hivyo tulilazimika kufanya kazi zilizokuwa za nguvu kwani
elimu wakipata watu wenye hadhi na muonekano maalumu ambao ni wenye uwezo wa
kifedha na kiutawala hukuwao wakifanya kazi za kitwana ikiwemo ulinzi na
ukulima”amesema Bwana Khamis.
Mwalimu mstaafu wa skuli ya sekondari ya Tumekuja amesema
kuwa miaka 62 ya mapinduzi ya Zanzibar imeleta mabadiliko makubwa katika sekta
ya elimu ambapo kuna ongezeko kubwa la maskuli yakiwemo ya horofa na kupelekea
kuongezeka kwa ufaulu kwa wanafunzi na kupelekea kupata maendeleo makubwa.
“Miaka 62 ya mapinduzi ya Zanzibar imeleta mabadiliko
makubwa katika sekta ya elimu ambapo kuna ongezeko kubwa la maskuli yakiwemo ya
horofa na kupelekea kuongezeka kwa ufaulu kwa wanafunzi na kupelekea kupata
maendeleo makubwa”amesema Mwalim
Mwanafunzi wa Kidatu cha nne katika skuli ya sekondari ndugu
Khadija Juma amesema kuwa wanaishukuru serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa
kuwapatia elimu bora yenye manufaa bila ya ubaguzi ambapo ndio lengo halisi la
mapinduzi ya mwaka 1964 la elimu bora kwa wote.
“Tunaishukuru serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa
Daktari Hussein Mwinyi kwa kutufanikisha kusoma bila ya ubaguzi ambao hata sisi
watoto wa wakulima na wakwezi tunasoma bila ya kikwazo chochote na kufanikisha
kupata elimu bora bila ya ubaguziambapo ni tofauti na kabla ya mapinduzi ya
mwaka 1964” amesema mwanafunzi huyo.
Sekta ya elimu ndio chachu ya maendeleo katika nchi, hivyo
basi ni vyema kwa wananchi kuyashukuru na kuyalinda mapinduzi ya 1964 ya
Zanzibar ili yaweze kudumu na kuhakikisha kila mtoto wa mkwezi na mkulima
anasoma sawa na mtoto wa tajiri bila yaubaguzi wa aina yoyote kwani miaka 62 ya
mapinduzi imeleta taswira nzuri katika sekta ya elimu.
Mafanikio makubwa ambayo nchi inajivunia ni kuendelea kuwepo
kwa amani nchini. Hii ni nguzo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa mipango
yote ya maendeleo na ustawi wa Taifa. Ni vyema kusisitiza umuhimu wa kuitunza
amani na kuendelea kuwa wamoja na wenye mshikamano. Kwa kufanya hivyo, nchi
itazidi kupiga hatua kubwa zaidi za maendeleo tunayoyatarajia kwa faida watu wote.Kwani
bila ya Amani nchi haiwezi kupata maendeleo.




No comments