Breaking News

VIJANA WATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WENYE SIFA.

 


Na Siti Ali,

Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji  Mhe, Shaaban Ali  Othman amewataka  vijana kuchagua viongozi wenye uwezo na sifa ya   kuwasimamia Vijana wenzao kuanzia  ngazi ya Shehia .

Ameyasema hayo  katika muendelezo wa ziara ya kuzungumza na Vijana huko Uwanja wa Granada Welezo Wilaya ya Magharibi 'A'

Amesema uchaguzi utakaofanyika uwe wa huru na haki sambamba na uadilifu katika kuchagua viongozi ambao watakuwa ni sauti ya kuwasemea changamoto zao sambamba na kuimarisha uhai Mabaraza ya Vijana Katika ngazi ya Shehia Wilaya hadi Taifa 

 Aidha amesema Wizara hiyo imejipanga kuzalisha Ajira mbali mbali ikiwemo ajira za Serikali Sekta binafsi,pamoja na  kupatiwa fedha za  kujiendeleza katika kuimarisha  mitaji ya Biashara zao 

Amewataka Vijana kutokubali kutoa rushwa  katika Masuala ya ajira kwani Serikali wala sekta binafsi haitoi ajira kwa fedha hivyo kutoa rushwa ni kosa kisheria .



Ameeleza  kwamba Wizara itahakikisha inazalisha Ajira na kuwaletea Vijana ili kuendelea kuwa raia wema   katika nchi yao na kuona Ustawi wao unaimarika.

Nae Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Ali Haji Hassan amewataka Vijana waendelee kuwahamasisha Vijana wenzao ili waweze kuitumia fursa ya kuchagua na kuchaguliwa  katika Uchaguzi wa Mabaraza ya Vijana .

Kwa Upande wa Kamishna wa Kinga Tiba na Marekebisho ya Tabia kutoka Mamlaka ya dawa za kulevya Juma Abraham Zidikheir amesema waathirika wakubwa wa madawa ya kulevya ni Vijana ambao hupata matatizo  ya afya ya akili .

Ameeleza kuwa baadhi  ya Watumiaji wa uraibu  hupoteza ajira,afya ya mwili  sambamba na kuathiri familia zao kupata vifungo vya muda mrefu pamoja na kutaifishwa mali zao.


No comments