Breaking News

SERIKALI KUTEKELEZA SERA YA MAJI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI VIJIJINI.

 


Na Fatma Rajab.

Seriklai itaendelea kutekeleza sera ya maji na usafi  wa mazingira kwa lengo  la kuhakikisha kunapatikana maji safi na salama katika jamii pamoja na kupunguza utegemezi wa nishati ya umeme.

Hayo yameelezwa na waziri wa nchi afisi ya Rais Mhe: Saada Mkuya Salum wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji huko nungwi kilindi  mkoa wa kaskazini unguja. 

Aidha amewataka vijana kuwa walinzi wakbwa wa kulinda miundombinu hiyo na kuacha tabia ya kufanya uharibifu wa maji. 

Nae katibu mkuu Wizara ya Maji Nishati na Madini Zanzibar Mhe Joseph John  Kilangi  akitoa taarifa ya kitaalamu kuhusina na mradi huo amesema kuwa, mradi huo ulianza Septmba 23 na ujenzi ulianza mwezi wa April 2024 na ulipangwa umalizike 2025 lakini kutokana na changamoto mbali mbali ilibidi uongeewe mda hadi Juni 2026. 

Mradi huo una jumla ua skimu 4 machumi, kilindi,  kiwengwa na Nungwi lengo ikiwa ni kuondoa kero ya maji katika jamii.

Pia amesma katika mradi huo kutakuwa na matengenezo ya visima vitatu pmoja na kuboresha visima vya zamani kwa kuweka umeme wa nishati ya  jua ili kuhakikisha kila mwanachi anapata maji kwa muda muafaka.

Kwa upande wake Rashid simai msaraka akizungumza kwa niaba ya  mkuu wa mkoa wa kaskazini Unguja amesema, miundo mbinu inayoletwa katika  mkoa wa nungwi imekuwa ikisaidia kukuza sekta ya utalii kwa kiasi kikubwa 

Sambamba na hayo amaeckuwa fursa hiyo kwa kutoa shukrani kwa wizara ya maji kwa kuhakikusha wanajenga miradi ya maji katika kila kijiji katika mji wa zanzibar kwani maji ni kitu muhimu sana katika jamii.

Nao wananchi wa kijiji cha nungwi wamesama kuwa wanashukuru serikali kwa kuwaletea maji katika kijiji chao na wameahidi kuitunza miundo mbinu hiyo ili iweze kudumu kwa vizazi vya sasa na baadae na endapo wataona mtu anafnya uharibifu juu ya huduma za maji basi watachkuwa hatua zinazostahiki ili kuhakikisha wanadumisha rasilimali hiyo.


No comments