Breaking News

"FUATENI SHERIA NA MIONGOZO YA UVUVI" AFISA UVUVI WILAYA YA KATI.



Wavuvi wa Ghuba ya Chwaka wametakiwa kuendelea kufuata sharia na taratibu ziloekwa kwa mujibu wa sharia No. 7 ya mwaka 2010 ili kuwa na rasilimali endelevu kwa manufaa yao na kizazi kijacho.

Wito huo umetolewa na Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Kati Unguja Ali Mwalim Mahafoudh kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar wakati wa mafunzo ya siku mbili huko Dunga juu ya uvuvi haramu unavoathiri kwenye maeneo ya hifadhi za bahari.

Afisa huyo amesema lengo la mafunzo hayo kuwanasihi wavuvi wenye kujishughulisha na uvuvi wa nyavu za kukokota,madema ya waya na matumizi ya sumu ya utupa kuachana na uvuvi huo ili kukuza kipato chao kupitia rasilimali za bahari.

Sambamba na hilo amesema Serikali ipo mbioni kuendelea na mpango wa kutoa boti kwa awamu ya pili kwa wavuvi ili kuondokana na uvuvi wa maji ya ndani na kuenda kuvua nje ya  maeneo ya hifadhi za bahari .

Kwa upande wao Washiriki wa mafunzo hayo Nd.Maulid Faki Hindi kutoka Pongwe ameishukuru Serikali kwa kuwapatia elimu kutokana na kuwepo kwa baadhi ya wavuvi bado wanaendelea uvuvi haramu jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi ya usimamizi wa rasilimali za bahari .

Nae Vuwaa Muhidini Mcha Mvuvi kutoka Chwaka amesema mafunzo haya yamewasaidia kwa kiasi kikubwa hivyo ameomba kuwe na mashirikiano kati ya wavuvi kamati na Taasisi husika kwa ajili ya  kupata uwelewa zaidi uvuvi unaokubalika kisheria.

Vilevile Mvuvi Said Ali kutoka Shehia ya Uroa ameiomba Serikali kuwapatia nyezo za uvuvi na wapo tayari kuachana na uvuvi haramu kutokana na sharia na kanuni zinawaka  kufanya hivyo.

Kwa upande wake Khamis Haji Khamis kutoka Ukongoroni ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Uchumi wa buluu na uvuvi kuwawezesha boti na vifaa vyake vya kuvulia kutokana na wavuvi walio wengi hali zao ni duni kimaisha.

Mafunzo hayo yametayarishwa na Idara ya Maendeleo ya uvuvi na mazao ya baharini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mwambao MCCC zaidi ya Wavuvi 46 kutoka shehia ya Uroa ,Chwaka , Ukongoroni Charawe na Pongwe wamepatiwa mafunzo ya uvuvi usiokubalika kisheria baharini .


No comments