WATOTO WAWILI WA FAMILIA MOJA WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA MOTO.
Na Mwandishi wetu.
Watoto wawili wamepoteza maisha baada ya moto kuteketeza nyumba waliyokuwa wakiishi katika Mtaa wa Katanini, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na vyombo vya habari, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomaji, amesema watoto hao ni wana wa wakili wa kujitegemea, Caessar Shayo.
Watoto waliopoteza maisha ni Jerial Shayo miaka (4) na Leoni Shayo miaka (2), pia moto huo ulisababisha majeruhi wawili baba na mama wa watoto hao na kwa sasa wanapatiwa matibabu rufaa ya Kanda ya kaskazini,"amesema Kaimu Kamanda Zimamoto.
Kamanda Jeremiah amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa nne asubuhi, ambapo kwa mujibu wa mashuhuda, watoto hao walifariki dunia muda mfupi baada ya kupewa uji na dada wa kazi.
Naye, Mwenyekiti wa Mtaa wa Katanini, Ester Mekiesia, amesema alipokea taarifa za moto huo kutoka kwa wananchi na mara moja alichukua jukumu la kutoa taarifa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kuokoa hali hiyo.

No comments