RAIS Samia Suluhu Hassan ameongoza familia, katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho
RAIS Samia Suluhu Hassan ameongoza familia, viongozi, wabunge na waombolezaji wengine, katika ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Joakim Mhagama, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mwenyeheri Maria-Theresa Ledochowska, Parokia ya Kiwanja cha Ndege, Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, leo Desemba13, 2025.
Akizungumza katika ibada hiyo kuhusu Jenista Rais Samia amesema: “Umetimiza wajibu wako kwa uaminifu mkubwa. Umepigana vita vilivyokupasa. Uimara wa taifa letu ni pamoja na mchango wako mkubwa. Mwenyezi Mungu akupe safari ya heri, safari njema, ailaze roho yako mahali pema peponi, amina. Sote kwa Imani zetu tunamuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yako kwa amani milele na milele”
Mwili wa Jenista Mhagama, utaagwa na wananchi wa Jimbo la Peramiho kwa kutoa heshima zao za mwisho katika ibada itakayofanyika Desemba 14, 2025 kwenye Kanisa Katoliki Peremiho, ambapo Desemba 16, 2025 mwili wake utazikwa katika kijiji cha Ruanda, Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
No comments