Breaking News

MATUKIO YA UDHALILISHAJI YAONGEZEKA KWA MWEZI WA NOVEMBA 2025, WADAU WATOA RAI.



 Na Said Khamis.

Idadi ya matukio ya udhalilishaji imeongezeka kwa mwezi Novemba ikilinganishwa na mwezi Oktoba mwaka huu 2025.

Akitoa Taarifa katika mkutano na waandishi wa Habari Ndugu Ahmada Hassan Suleiman kutoka Divisheni ya Jinsia na Ajira Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar amesema matukio ya mwezi Novemba yamefikia 107 ikilinganishwa na matukio 99 ya mwezi Oktoba mwaka huu, huku akieleza kuwa matukio ya ubakaji yameshika kasi kutoka 47 Mwezi Oktoba Hadi 59 mwezi Novemba.

Amesema kati ya matukio 59 ya kubaka yaliyoripotiwa kwa Mwezi Novemba 2025 matukio Tisa yameripotiwa Wanawake na asilimia 15.3 na matukio 50 yameripotiwa kwa wasichana sawa na asilimia 84.7

Amesema Wilaya Wete imeripotiwa kuwa na Idadi kubwa ya matukio ya ubakaji ikilinganishwa na Wilaya nyengine ambayo Jumla ya matukio ya kubaka 10 sawa na Asilimia 16.9 kati ya matukio yote ya kubaka yaliyoripotiwa.



Akitoa ufafanuzi juu ya sababu zinazopelekea kuongezeka kwa matukio ya udhalilishaji Inspekta wa Polisi Makame Haji kutoka Makao Makuu ya Polisi zanzibar amesema uhuru Mkubwa uliopitiliza wa Wazazi kwa watoto wao hatua inayopelekea watoto hao kufanya lolote wanalolitaka pasi na kuwa na wasi wasi wa vitendo wanavyovifanya.

Amewaasa jamii kutoa Taarifa za udhalilishaji mara baada ya kutokea kwa matukio hayo ili kulinda ushahidi wa awali hatua inayopelekea kukamilika kwa haraka kwa kesi hizo



Nae Ndugu Fatma Serembe Khamis kutoka Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora ameeleza kuwa ili kupunguza vitendo vya udhalilishaji Nchini Tume imekubaliana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuanzisha program ndani ya maskuli ili kutoa Elimu kwa Wanafunzi juu ya dhana nzima na namna ya kujilinda na udhalilishaji.


No comments