Breaking News

91 WAZAWADIWA MTAMBILE KWA KUPASI MICHEPUO.



Na Mwandishi wetu,

Mbunge wa Jimbo la Mtambile, amekabidhi zawadi kwa wanafunzi 91 waliopasi michepuo katika mitihani ya darasa la 7.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa wanafunzi hao  iliyofanyika katika ukumbi wa skuli ya sekondari Mtambile Mbunge wa Jimbo hilo  Said Ibrahim Mzimba,  amesema kuwa zawadi hizo ni ishara ya kuthamini juhudi za wanafunzi na kuwahamasisha kuendelea kujituma katika masomo yao.

Amesema kuwa chama cha ACT Wazalendo kinaamini katika elimu kama njia ya kuendeleza maisha ya watu na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Pia Mbunge huyo amesema ni matarajio yake kuona wanafunzi hao wakifanya vizuri zaidi katika masomo yao na kuwa viongozi bora wa baadaye.

Kwa upende wake Mwalimu Mkuu Skuli ya Mjimbini Nasra Ali Omar,  amesema kuwa zawadi hizo ni ishara ya kuthamini juhudi za wanafunzi hao na kuwahamasisha kuendelea kujituma katika masomo yao.

Aidha amewataka wazazi na walezi kuweka mazoeya ya karibu na watoto wao ili kugundua changamoto wanazozipitia katika masomo yako.

Nae Mwenyekiti wa ACT Jimbo la Mtambile Sharif Salim Ali,  amesema zawadi hizo ni miongoni mwa ahadi zilizowekwa na chama chake wakati wa kuomba ridhaa  kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa 2025.



 Amesema chama cha ACT wazalendo kitaendelea kuwapa zawadi wanafunzi wate watakao faulu masomo ya darasa la 7 na kidato cha 4 kila mwaka,  lengo ni kuongeza hamasa ya wanafunzi na kuwapunguzia mzigo wazazi na walezi katila kusomesha watoto wao.

Zawadi zilizokabidhiwa kwa wanafunzi hao ni pamoja na Magodoro, Mikoba, Mabuku, kampas,  kalamu  na sare za skuli ikiwa ni ahadi ya kuimarisha sekta ya elimu katika Jimbo la mtambile.


No comments