Breaking News

IIT MADRAS ZANZIBAR YAWEKA KITUO CHA PROGRAMU YA KIMATAIFA YA DATA SAYANSI, AKILI BANDIA NA USALAMA MTANDAO KWA WATAALAMU WA UKAGUZI

NA SITI ALI
Taasisi ya Teknolojia ya India Madras, Kampasi ya Zanzibar (IIT Madras Zanzibar – IITMZ), imekuwa mwenyeji wa programu ya mafunzo ya muda mfupi kuhusu Data Sayansi, Akili Bandia na Usalama Mtandao kwa wataalamu wa ukaguzi na uthibiti wa hesabu za serikali kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Programu hiyo ya wiki mbili imeasisiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa India (CAG) na kuandaliwa kwa pamoja na IIT Madras Zanzibar, ikiwa na lengo la kuwawezesha wataalamu wa ukaguzi kupata maarifa na ujuzi unaohitajika katika kutumia teknolojia za kisasa katika shughuli za ukaguzi.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa programu hiyo, viongozi mbalimbali walisisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia, hususan Data Sayansi, Akili Bandia na Usalama Mtandao, katika kuimarisha ufanisi na ubora wa ukaguzi wa hesabu za serikali katika mazingira ya sasa yanayobadilika kwa kasi kiteknolojia.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi na wageni mbalimbali mashuhuri, akiwemo Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Afisa Mkuu wa Teknolojia wa Ofisi ya CAG ya India, Mhe. Bijay Kumar Mohanty, pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Charles E. Kichere, na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar, Dk. Othman Abass Ali.
Wengine waliohudhuria ni Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey, Balozi Mdogo wa India Zanzibar, Mhe. Sarjeet Kajla, pamoja na Mkuu wa Taaluma wa IIT Madras Zanzibar, Prof. Akkihebbal K. Suresh, ambao walishiriki katika kuunga mkono juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma na kiteknolojia kati ya India na nchi za Afrika.
Programu hiyo imewakutanisha jumla ya washiriki 30 kutoka nchi nane za Afrika ambazo ni Algeria, Egypt, Tunisia, Liberia, Morocco, Mauritius, Gambia na Tanzania. Washiriki hao wanapata fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu namna teknolojia mpya zinavyoweza kutumika katika kuboresha michakato ya ukaguzi na uthibiti wa matumizi ya fedha za umma.
Kupitia mafunzo hayo, washiriki wanajengewa uwezo katika matumizi ya Data Sayansi, Akili Bandia na Usalama Mtandao katika shughuli za ukaguzi, sambamba na kujenga mitandao ya kitaaluma na kubadilishana uzoefu kuhusu changamoto zinazotokana na mabadiliko ya teknolojia katika sekta ya ukaguzi.
Programu hiyo inaonesha dhamira ya IIT Madras Zanzibar katika kukuza ushirikiano wa kimataifa, kujenga uwezo wa wataalamu wa Afrika na kuhamasisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika kuimarisha taaluma ya ukaguzi. Ushirikiano huo pia unatoa fursa k


No comments