Breaking News

WAZAZI MUNAJUKUMU LA KUSIMAMIA MAENDELEO YA ELIMU YA WATOTO WENU :MUSSA.

 Na Said Khamis


‎Wazazi na Walezi wametakiwa kuwa na utamaduni wa kufuatilia maendeleo ya Watoto wao katika masomo pamoja na kuwafundisha  Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.
‎Hayo ameyasema Mkuu wa Divisheni ya Mapato, Uchumi na Wajasiriamali Baraza la Manispaa Kati Mussa Abdurab Fadhil katika Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Manispaa Kati Dunga Wilaya ya Kati Unguja.
‎Amesema jukumu la kuwafunza  Watoto sio la Walimu pekee kwani hata Mzazi anawajibu wakumfundisha Mtoto kuhakikisha anajua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu nambari.


‎Mussa alisema kwamba endapo mwalimu hatotimiza wajibu wake katika kumsomesha mtoto  atakua amemfanyia udhalilishaji mwanafunzi kwa kumkosesha kupata haki yake ya elimu.
‎Kwa upande wake Afisa Elimu Wilaya ya Kati Somoe Said Mussa amesema Mtoto anahaki mbalimbali katika jamii ambazo anahitaji kupatiwa ikiwemo Kulindwa, Kuthaminiwa pamoja na kupatiwa elimu bila ya ubaguzi wowote.

‎Ameeleza kuwa maadhimisho hayo wameadhimisha kwa michezo mbalimbali ya watoto ikiwemo mchezo wa citi, ngonjera, utenzi nyimbo mbalimbali na hata kufanya maandamoano.
‎Nae Mwalimu wa Skuli ya Maandalizi Binguni Khadija Mshimba Makame amewaomba Wazazi kuwa karibu na Watoto wao hususani wanaporudi nyumbani ili kuepukana na  udhalilishaji wa kijinsia.
‎Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afirika huadhimishwa kila ifikapo  Tarehe 16 mwezi 6 kila mwaka na kauli mbiyu ya mwaka huu inasema Linda Mtoto wa Afrika, Afya bora na Maisha bila ya udhalilishaji.

1 comment:

  1. Mtoto ana haki nyingi, tujitahidi kuzitimiza

    ReplyDelete