Breaking News

WATOTO YATIMA WAASWA KUZINGATIA MASOMO.



 Na Said Khamis‎.
‎Wtoto yatima wametakiwa kuwa na matumaini na kuweka bidii katika masomo yao ili kuja kuwa raia wema na wenye tija katika Jamii.
‎Wito huo umetolewa na Diwani wa Wadi ya Melinne, Swaleh Juma Kinana,  katika hafla maalum ya dua na chakula cha pamoja iliyoandaliwa na Jumuiya ya Al-Taqwa Foundation huko Uwanja wa Ndege Mjini Unguja.

‎Kinana alisema mtoto yatima ana daraja kubwa mbele ya Allah SW hivyo kuna kila sababu kwa jamii kuwapigania watoto hao  kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya kimaisha.‎
‎"Ni vyema jamii ikasimama kidete kuwapigania watoto hawa katika kutimiza malengo yao ya baadae, kuwa yatima sio uonevu, na hawa watoto wana daraja kubwa sana," alisema Diwani Kinana

‎Akisoma risala katika hafla hiyo, Juma Amour Khamis ameeleza kuwa watoto yatima wengi wanaishi katika mazingira magumu na wanahitaji mahitaji muhimu ili kuendesha maisha yao. 
‎Alieleza kuwa Jumuiya hiyo ya Al-Taqwa, ambayo sasa imetimiza miaka sita tangu kuanzishwa kwake, imekuwa ikisaidia watoto yatima na maskini wenye hali duni.
‎Akizungumzia changamoto zinazoikabili Jumuiya hiyo Khamis ameleza kuwa changamoto kubwa ni uwepo kwa uhaba wa michango na ukosefu wa usafiri wa kuwafikia walengwa kwa urahisi.





‎Aliongeza kuwa jumuiya hiyo ina mpango wa kujenga ofisi yao wenyewe ili kuendeleza na kutanua shughuli zao za kibinadamu.
‎Nao baadhi ya watoto yatima walioshiriki katika dua na chakula hicho cha mchana wameishukuru taasisi hiyo kwa upendo wao, kuwa karibu nao, na kuendelea kuwapatia mahitaji yao muhimu ya kila siku.



‎"Jumuiya ya Al-Taqwa Foundation siku hii yaleo imetuunga mkono katika kutupatia chakula cha mchana pamoja na kuwaombea dua wazee wetu waliotangulia mbele ya haki tunawashukuru kwa msaada huo " walisema watoto hao
‎Zaidi ya watoto yatima 150 wamejumuika pamoja katika dua hiyo na sadaka hiyo ya chakula yenyelengo la kuimarisha umoja na mshikamano.

1 comment: