Breaking News

JAMII YAHIMIZWA KUHIFADHI MAZINGIRA YA BAHARI KWA MASLAHI ENDELEVU.

 


NA SAID KHAMIS

 Shehia sita za Wilaya ya Kusini zimetakiwa kuwa na jukumu la kuisimamia jamii juu ya kuachana na uchafuzi wa bahari kwa maslahi ya Wavuvi na Taifa kwa ujumla.


Akizungumza  kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Uhifadhi wa Bahari Zanzibar   Mkuu wa Divisheni wa uhifadhi Shirikishi Jamii  Mchanga Said Khamis kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi  wakati wa uzinduzi wa Mradi wa usimamizi wa rasilimali za bahari huko katika ukumbi wa ZAFIRI Maruhubi.



Mkuu huyo alisema kuwepo kwa usimamizi mzuri wa rasilimali za bahari ni chachu ya maendeleo kwa Wavuvi kutokana na utunzaji wa bahari pamoja na kuimarika  kwa rasilimali hizo.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Zanzibar Ndugu Sharifa Mohammed Miraji aliziomba Kamati za Uvuvi kuhamasisha jamii kuunga mkono zoezi la Sensa ya uvuvi itayaofanyika hivi karibuni ili Serikali iweze kutambua mahitaji ya wavuvi nchini.



Nao Wasimamizi wa Miradi kutoka Taasisi ya  Marine Culture Ndugu Ali Mahmoud na Ndugu Gabriel Masala walielezea kuwa wapo tayari kuisaidia jamii ya ukanda wa pwani katika kusimamia rasilimali za bahari kwa njia endelevu kwa maslahi ya kizazi cha sasa na baadae.
Sambamba na hilo  walitoa wito kwa jamii husika kuunga mkono juhudi za miradi ya usimamizi wa rasilimali za bahari ili ileta tija kwa Wananchi.



Aidha walisema kuwa usimamizi wa rasilimali za bahari unatumia mifumo na utaratibu wa jamii ili kupata ufanisi mzuri wa usimamizi baharini.



Mkutano huo wa siku moja uliandaliwa na Idara ya Uhifadhi wa bahari na Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Zanzibar kwa kushirikiana na Taasisi ya Marine Culture iliopo Jambiani  na Kuzishirikisha Shehia ya Bwejuu, Paje, Jambiani Kibigija ,Kigadini, Kajengwa na Dongwe




1 comment: