Breaking News

AJIRA MPYA ZANUKIA SEKTA YA AFYA ZANZIBAR



Na siti Ali

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inakusudia kutoa kibali cha ajira mpya katika mwaka mpya wa fedha kwa sekta ya afya na kada nyingine ili kupunguza tatizo la uhaba wa wauguzi hapa nchini.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika Kongamano la Kwanza la Kisayansi la Wauguzi lililoambatana na Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani, yaliyofanyika Hoteli ya Verde.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea kukabiliana na changamoto za sekta ya afya, hususan upungufu wa wauguzi na madaktari, pamoja na kuimarisha miundombinu ya afya ikiwemo ujenzi wa Hospitali Mpya ya Mnazi Mmoja na Hospitali ya Saratani Binguni sambamba na upatikanaji wa vifaa vya kisasa.

Aidha, amewataka wauguzi kufanya kazi kwa moyo, huruma na weledi huku akipongeza maendeleo ya kitaaluma yaliyofikiwa na wauguzi katika kipindi cha miaka 62 ya Mapinduzi, kutoka ngazi ya stashahada hadi uzamivu.

Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani mwaka 2026 yamefanyika chini ya kauli mbiu isemayo “Kuwawezesha Wauguzi ni Kuokoa Maisha” (Empowering Nurses, Saving Lives).


No comments