Breaking News

ZANZIBAR KUIMARISHA ELIMU KIDIJITALI.



Na Said Khamis

Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mwl. Muhammed Nassor Salim amesema muelekeo wa serikali na wizara ya elimu ni kuimarisha elimu kwa kutumia tekolojia sambamba na matumizi ya mifumo ya kidijitali.

Kauli hiyo ameitoa kwa nyakati tofauti katika warsha maalum kwa Walimu Wakuu na Wasaidizi iliyofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Utaani Wilaya ya Kaskazini Pemba na Skuli ya Sondari Fidel Castro Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.

Amesema kwakua lengo la Serikali katika kipindi cha 2026 2030 ni kuhakikisha kuwa Zanzibar inakwenda vizur katika eneo la matumizi ya TEHAMA, Walimu hawanabudi kujiimarisha katika eneo hilo ili kutimiza lengo la Serikali.

Amesema Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar imewekeza nguvu kubwa katika kuwapatia Walimu Mafunzo wakiwa kazini sambamba  na Mafunzo ya TEHAMA ikiwa ni  pamoja na kuziunga Skuli na Mikonga wa Taifa kwa lengo la kuhama kutoka analogi kwenda digital.



Akitoa ufafanuzi zaidi Mwl. Moh’d amesema licha ya Changamoto zilizopo katika Skuli mbali mbali Walimu hawana budi kufanya kazi kwa bidii na kutafuta njia ya kutatua Changamoto hizo.

Katika Warsha hiyo Waratibu  wa Idara na Wakuu wa Vitengo wamwwasilisha Mada mbali mbali kwa Walimu hao.



Miongoni mwa mada zilizowasilishwa ni Ukaguzi wa ndani, Matumizi Sahihi ya fedha, Utatuzi wa Migogoro na Maadili.


No comments